Yobu 38:1-11
Yobu 38:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Hapo Mwenyezi-Mungu alimjibu Yobu kutoka dhoruba: “Nani wewe unayevuruga mashauri yangu kwa maneno yasiyo na akili? Jikaze kama mwanamume, nami nitakuuliza nawe utanijibu. “Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya dunia? Niambie, kama una maarifa. Ni nani aliyeweka vipimo vyake, wajua bila shaka! Au nani aliyelaza kamba juu yake kuipima? Je, nguzo za dunia zimesimikwa juu ya nini, au nani aliyeliweka jiwe lake la msingi, nyota za asubuhi zilipokuwa zikiimba pamoja, na wana wa Mungu wakapaza sauti za shangwe? Ni nani aliyeyafunga mafuriko ya bahari wakati yalipozuka na kuvuma kutoka vilindini? Mimi ndiye niliyeifunika bahari kwa mawingu na kuiviringishia giza nene. Niliiwekea bahari mipaka, nikaizuia kwa makomeo na milango, nikaiambia: ‘Mwisho wako ni hapa, si zaidi! Mawimbi yako ya nguvu yatakomea hapa!’
Yobu 38:1-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema, Ni nani huyu atiaye ushauri giza Kwa maneno yasiyo na maarifa? Basi jifunge viuno kama mwanamume, Maana nitakuuliza neno, nawe niambie. Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama una ufahamu. Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake – hakika unajua! Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake? Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni, Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha? Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango, Hapo ilipotoka kwa nguvu kama kwamba imetoka tumboni mwa nchi. Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake, Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia, Nikaiagiza amri yangu; Nikaiwekea makomeo na milango, Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita, Na hapa mawimbi yako yenye nguvu yatazuiliwa?
Yobu 38:1-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema, Ni nani huyu atiaye mashauri giza Kwa maneno yasiyo na maarifa? Basi jifunge viuno kama mwanamume, Maana nitakuuliza neno, nawe niambie. Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu. Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua? Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake? Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni, Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha? Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango, Hapo ilipofurika kana kwamba imetoka tumboni. Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake, Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia, Nikaiagiza amri yangu; Nikaiwekea makomeo na milango, Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita, Na hapa mawimbi yako yanyetayo yatazuiliwa?
Yobu 38:1-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kisha BWANA akamjibu Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli. Akasema: “Nani huyu atiaye mashauri yangu giza kwa maneno yasiyo na maarifa? Jikaze kama mwanaume; nitakuuliza swali, nawe unijibu. “Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia? Niambie, kama unafahamu. Ni nani aliyeweka alama vipimo vyake? Hakika wewe unajua! Ni nani aliyenyoosha kamba ya kupimia juu yake? Je, misingi yake iliwekwa juu ya nini, au ni nani aliyeweka jiwe la pembeni, wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, na malaika wote walipokuwa wakishangilia kwa furaha? “Ni nani aliyeifungia bahari milango ilipopasuka kutoka tumbo, nilipoyafanya mawingu kuwa vazi lake, na kuyafungia katika giza nene, nilipoamuru mipaka yake, na kuiweka milango yake na makomeo mahali pake, niliposema, ‘Unaweza kufika hapa, wala si zaidi; hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea’?