Yobu 37:14-16
Yobu 37:14-16 Biblia Habari Njema (BHN)
“Unapaswa kusikiliza Yobu; nyamaza, usikilize maajabu ya Mungu. Je, wajua jinsi Mungu anavyovipa amri yake, na kufanya umeme wa mawingu yake ungae? Je, wajua jinsi mawingu yanavyoelea angani? Ndizo kazi za ajabu za yule aliye mkamilifu wa maarifa!
Yobu 37:14-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sikiliza neno hili, Ee Ayubu; Simama kimya, uzifikiri kazi za Mungu za ajabu. Je! Wajua wewe jinsi Mungu anavyoziagiza, Na kuufanya umeme wa wingu lake uangaze? Je! Wajua jinsi mawingu yalivyowekwa sawasawa, Hizo kazi za ajabu za huyo mkamilifu wa maarifa?
Yobu 37:14-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Sikiliza neno hili, Ee Ayubu; Simama kimya, uzifikiri kazi za Mungu za ajabu. Je! Wajua wewe jinsi Mungu anavyoziagiza, Na kuumulikisha umeme wa wingu lake? Je! Wajua jinsi mawingu yalivyowekwa sawasawa, Hizo kazi za ajabu za huyo mkamilifu wa maarifa?
Yobu 37:14-16 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Ayubu, sikiliza hili; nyamaza na uyafikiri maajabu ya Mungu. Je, unajua jinsi Mungu anavyoyaongoza mawingu, na kufanya umeme wake wa radi utoe mwanga? Je, wajua jinsi mawingu yanavyokaa yakiwa yametulia, hayo maajabu yake yeye aliye mkamilifu katika maarifa?