Yobu 33:8-22
Yobu 33:8-22 Biblia Habari Njema (BHN)
Kweli umesema, nami nikasikia; nimeyasikia yote uliyosema. Wewe umesema, u safi na wala huna kosa, u safi kabisa na huna hatia; umesema kwamba Mungu anakutafutia kisa, na kukuona kama adui yake. Anakufunga miguu minyororo, na kuchunguza hatua zako zote. “Lakini Yobu, nakuambia hapo umekosea. Mungu ni mkuu kuliko binadamu. Kwa nini unashindana naye, ukisema hatajibu swali lako moja? Mungu anaposema hutumia njia moja, au njia nyingine lakini mtu hatambui. Mungu huongea na watu katika ndoto na maono, wakati usingizi mzito unapowavamia, wanaposinzia vitandani mwao. Hapo huwafungulia watu masikio yao; huwatia hofu kwa maonyo yake, wapate kuachana na matendo yao mabaya, na kuvunjilia mbali kiburi chao. Hivyo humkinga mtu asiangamie shimoni, maisha yake yasiangamie kwa upanga. “Mungu humrudi mtu kwa maumivu yamwekayo kitandani, maumivu hushika viungo vyake bila kukoma; naye hupoteza hamu yote ya chakula, hata chakula kizuri humtia kinyaa. Mwili wake hukonda hata asitambuliwe, na mifupa yake iliyofichika ikatokeza nje. Yuko karibu sana kuingia kaburini, na maisha yake karibu na wale waletao kifo.
Yobu 33:8-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hakika umenena masikioni mwangu, Nami nimesikia sauti ya maneno yako, ukisema, Mimi ni safi, sina makosa; Sina hatia, wala hapana uovu ndani yangu; Tazama, yuaona sababu za kufarakana nami, Hunihesabu kuwa ni adui yake; Hunitia miguu yangu katika mkatale, Na mapito yangu yote huyapeleleza. Tazama, nitakujibu, katika neno hili huna haki; Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu. Kwa nini unapingana naye, ukisema, Hatajibu hata neno langu moja? Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ijapokuwa mtu hatambui. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiapo watu, Katika usingizi kitandani; Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia mhuri mafundisho yao, Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga. Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake; Hata roho yake huchukia chakula, Na nafsi yake huchukia nyama nzuri. Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane; Na mifupa yake isiyoonekana yatokeza nje. Naam, nafsi yake inakaribia shimoni, Na uhai wake unakaribia waangamizi.
Yobu 33:8-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hakika umenena masikioni mwangu, Nami nimesikia sauti ya maneno yako, ukisema, Mimi ni safi, sina makosa; Sina hatia, wala hapana uovu ndani yangu; Tazama, yuaona sababu za kufarakana nami, Hunihesabu kuwa ni adui yake; Hunitia miguu yangu katika mkatale, Na mapito yangu yote huyapeleleza. Tazama, nitakujibu, katika neno hili huna haki; Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu. Nawe kwani kumnung’unikia, Kwa vile asivyotoa hesabu ya mambo yake yote? Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga. Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake; Hata roho yake huchukia chakula, Na nafsi yake huchukia nyama nzuri. Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane; Na mifupa yake isiyoonekana yatokea nje. Naam, nafsi yake inakaribia shimoni, Na uhai wake unakaribia waangamizi.
Yobu 33:8-22 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Lakini umesema nikiwa ninakusikia, nami nilisikia maneno yenyewe: ‘Mimi ni safi na sina dhambi; mimi ni safi na sina hatia. Lakini bado Mungu amepata dosari kwangu, naye ananiona kama adui yake. Ananifunga miguu kwa pingu, tena anaziangalia njia zangu zote kwa karibu.’ “Lakini mimi ninakuambia, katika jambo hili wewe una makosa, kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu. Kwa nini unamlalamikia kwamba yeye hamjibu mwanadamu? Kwa kuwa Mungu husema, wakati huu kwa njia moja, au wakati mwingine kwa njia nyingine, ingawa mwanadamu anaweza asielewe. Mungu husema na mwanadamu katika ndoto, katika maono ya usiku, wakati usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu wasinziapo vitandani mwao, anaweza akasemea masikioni mwao, na kuwatia hofu kwa maonyo, ili kumgeuza mtu kutoka kutenda mabaya na kumwepusha na kiburi, kuiokoa nafsi yake na shimo, uhai wake usiangamizwe kwa upanga. Mtu anaweza kutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, kwa dhiki za mfululizo katika mifupa yake, kiasi kwamba maisha yake yenyewe yanakataa chakula nayo nafsi yake ikakichukia kabisa hata chakula kizuri. Nyama ya mwili wake huisha kwa kukonda, nayo mifupa yake ambayo mwanzoni ilikuwa imefichika, sasa inatokeza nje. Nafsi yake inakaribia kaburi, nao uhai wake karibu na wajumbe wa kifo.