Yobu 33:1-3
Yobu 33:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
“Sasa, Yobu, sikiliza hoja yangu; sikiliza maneno yangu yote. Tazama, nafumbua kinywa changu, naam, ulimi wangu utasema. Nitasema kadiri ya unyofu wa moyo wangu; ninayoyajua nitayasema kwa uaminifu.
Yobu 33:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini, Ayubu, nakuomba usikilize hoja yangu, Ukayasikilize maneno yangu yote. Tazama basi, nimefunua kinywa changu, Ulimi wangu umenena kinywani mwangu. Maneno yangu yatatamka uelekevu wa moyo wangu; Na hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu.
Yobu 33:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Walakini, Ayubu, nakuomba usikilize matamko yangu, Ukayasikilize maneno yangu yote. Tazama basi, nimefunua kinywa changu, Ulimi wangu umenena kinywani mwangu. Maneno yangu yatatamka uelekevu wa moyo wangu; Na hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu.
Yobu 33:1-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Lakini Ayubu, sasa, sikiliza maneno yangu; zingatia kila kitu nitakachosema. Karibu nitafungua kinywa changu; maneno yangu yapo katika ncha ya ulimi wangu. Maneno yangu yanatoka katika moyo mnyofu; midomo yangu hunena kwa uaminifu yale niyajuayo.