Yobu 24:13-17
Yobu 24:13-17 Biblia Habari Njema (BHN)
“Wapo wengine waovu wasiopenda mwanga, wasiozifahamu njia za mwanga, na hawapendi kuzishika njia zake. Mwuaji huamka mapema alfajiri, ili kwenda kuwaua maskini na fukara, na usiku ukifika, kazi yake ni kuiba. Mzinifu naye hungojea giza liingie; akisema, ‘Hakuna atakayeniona;’ kisha huuficha uso wake kwa nguo. Usiku wezi huvunja nyumba, lakini mchana hujifungia ndani; wala hawajui kabisa mwanga ni nini. Kwao wote giza nene ni mwanga wa asubuhi; wao ni marafiki wa vitisho vya giza nene.
Yobu 24:13-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hawa ni katika hao waliouasi mwanga; Hawazijui njia zake, Wala hawakai katika mapito yake. Mwuaji huamka asubuhi kukipambazuka, huwaua maskini na wahitaji; Tena wakati wa usiku yu kama mwizi. Tena jicho lake mzinifu hungojea wakati wa gizagiza, Akisema, Hapana jicho litakaloniona; Naye huuficha uso wake. Wao hutoboa nyumba gizani; Hujifungia ndani wakati wa mchana; Hawaujui mwanga. Maana asubuhi kwao wote ni kama giza tupu; Maana wao wavijua vitisho vya hiyo giza tupu.
Yobu 24:13-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hawa ni katika hao waliouasi mwanga; Hawazijui njia zake, Wala hawakai katika mapito yake. Mwuaji huamka asubuhi kukipambauka, huwaua maskini na wahitaji; Tena wakati wa usiku yu kama mwivi. Tena jicho lake mzinifu hungojea wakati wa giza-giza, Akisema, Hapana jicho litakaloniona; Naye huuficha uso wake. Wao hutoboa nyumba gizani; Hujifungia ndani wakati wa mchana; Hawaujui mwanga. Kwani asubuhi kwao wote ni kama giza tupu; Kwani wao wavijua vitisho vya hiyo giza tupu.
Yobu 24:13-17 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Wako wale wanaoiasi nuru, wasiofahamu njia zake wala hawakai katika mapito yake. Mwanga wa mchana unapotoweka, muuaji huinuka, naye huwaua maskini na mhitaji; wakati wa usiku hunyemelea kama mwizi. Jicho la mzinzi hungojea wakati wa giza, naye hufikiri, ‘Hakuna jicho litakaloniona,’ naye huuficha uso wake. Katika giza, huvunja nyumba, lakini wakati wa mchana hujifungia ndani; hawataki kufanya lolote nuruni. Kwa wote hawa, giza nene ndiyo asubuhi yao; hujifanya rafiki na vitisho vya gizani.