Yobu 23:8-12
Yobu 23:8-12 Biblia Habari Njema (BHN)
“Tazama, nakwenda mbele, lakini simpati, narudi nyuma, lakini siwezi kumwona. Namtafuta upande wa kushoto lakini simwoni; nageukia kulia, lakini siwezi kumwona. Lakini yeye anajua njia ninayofuata; atakapomaliza kunijaribu nitatoka humo safi kama dhahabu. Nafuata nyayo zake kwa uaminifu njia yake nimeishikilia wala sikupinda. Kamwe sijaacha kushika amri yake, maneno yake nimeyatunza moyoni mwangu.
Yobu 23:8-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tazama, naenda mbele, wala hayuko; Narudi nyuma, lakini siwezi kumwona; Na mkono wa kushoto, afanyapo kazi, lakini siwezi kumwona; Hujificha upande wa kulia, hata nisimwone. Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka. Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu
Yobu 23:8-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tazama, naenda mbele, wala hayuko; Narudi nyuma, lakini siwezi kumwona; Na mkono wa kushoto, afanyapo kazi, lakini siwezi kumwona; Hujificha upande wa kuume, hata nisimwone. Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka. Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu
Yobu 23:8-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Lakini nikienda mashariki, hayupo; nikienda magharibi, simpati. Anapokuwa kazini pande za kaskazini, simwoni; akigeukia kusini, nako simwoni hata kidogo. Lakini anaijua njia niiendeayo; akiisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. Nyayo zangu zimefuata hatua zake kwa karibu; nimeishika njia yake bila kukengeuka. Sijaziacha amri zilizotoka mdomoni mwake; nimeyathamini maneno ya kinywa chake kuliko chakula changu cha kila siku.