Yobu 23:10-12
Yobu 23:10-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini yeye anajua njia ninayofuata; atakapomaliza kunijaribu nitatoka humo safi kama dhahabu. Nafuata nyayo zake kwa uaminifu njia yake nimeishikilia wala sikupinda. Kamwe sijaacha kushika amri yake, maneno yake nimeyatunza moyoni mwangu.
Yobu 23:10-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka. Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu
Yobu 23:10-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka. Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu
Yobu 23:10-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Lakini anaijua njia niiendeayo; akiisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. Nyayo zangu zimefuata hatua zake kwa karibu; nimeishika njia yake bila kukengeuka. Sijaziacha amri zilizotoka mdomoni mwake; nimeyathamini maneno ya kinywa chake kuliko chakula changu cha kila siku.