Yobu 22:21-27
Yobu 22:21-27 Biblia Habari Njema (BHN)
“Sasa, Yobu, kubaliana na Mungu uwe na amani, na hapo mema yatakujia. Pokea mafundisho kutoka kwake; na yaweke maneno yake moyoni mwako. Ukimrudia Mungu na kunyenyekea, ukiondoa uovu mbali na makao yako, ukitupilia mbali mali yako, ukaitupa dhahabu ya Ofiri ukingoni mwa kijito, Mungu Mwenye Nguvu akawa ndio dhahabu yako, na fedha yako ya thamani; basi, ndipo utakapomfurahia Mungu mwenye nguvu na kutazama kwa matumaini; utamwomba naye atakusikiliza, nawe utazitimiza nadhiri zako.
Yobu 22:21-27 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia. Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake, Na maneno yake yaweke moyoni mwako. Ukimrudia Mwenyezi, utajengwa; Ukiuondoa udhalimu mbali na hema yako. Nawe hazina zako ziweke mchangani, Na dhahabu ya Ofiri iweke kati ya mawe ya vijito; Naye Mwenyezi atakuwa hazina yako, Atakuwa ni fedha ya thamani kwako. Kwani ndipo utakapojifurahisha katika Mwenyezi, Na kuinua uso wako kumwelekea Mungu. Utamwomba yeye naye atakusikia; Nawe utazitimiliza nadhiri zako.
Yobu 22:21-27 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia. Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake, Na maneno yake yaweke moyoni mwako. Ukimrudia Mwenyezi, utajengwa; Ukiuondoa udhalimu mbali na hema yako. Nawe hazina zako ziweke mchangani, Na dhahabu ya Ofiri iweke kati ya mawe ya vijito; Naye Mwenyezi atakuwa hazina yako, Atakuwa ni fedha ya thamani kwako. Kwani ndipo utakapojifurahisha katika Mwenyezi, Na kuinua uso wako kumwelekea Mungu. Utamwomba yeye naye atakusikia; Nawe utazitimiliza nadhiri zako.
Yobu 22:21-27 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Mjue sana Mungu ili uwe na amani, ndipo mema yatakapokujia. Uyapokee mafundisho toka kinywani mwake, na maneno yake uyaweke moyoni mwako. Ukimrudia Mwenyezi, utarudishwa upya: Ukiuondoa uovu uwe mbali na hema lako, kama dhahabu yako ukiihesabu kama mavumbi, dhahabu yako ya Ofiri kama miamba ya mabondeni, ndipo Mwenyezi atakuwa dhahabu yako, naye atakuwa fedha yako iliyo bora. Hakika ndipo utakapojifurahisha kwa Mwenyezi, nawe utamwinulia Mungu uso wako. Utamwomba yeye, naye atakusikia, nawe utazitimiza nadhiri zako.