Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yobu 21:1-21

Yobu 21:1-21 Biblia Habari Njema (BHN)

Kisha Yobu akajibu: “Sikilizeni kwa makini maneno yangu; na hiyo iwe ndiyo faraja yenu. Nivumilieni, nami nitasema, na nikisha sema endeleeni kunidhihaki. Je, mimi namlalamikia binadamu? Ya nini basi, nikose uvumilivu? Niangalieni, nanyi mshangae, fumbeni mdomo kwa mkono. Nikifikiri yaliyonipata nafadhaika nafa ganzi mwilini kwa hofu. Kwa nini basi waovu wanaishi bado? Mbona nguvu zao zaongezeka hata uzeeni? Huwaona watoto wao wakifanikiwa; na wazawa wao wakipata nguvu. Kwao kila kitu ni salama bila hofu; wala kiboko cha Mungu hakiwafikii. Naam, ng'ombe wao wote huongezeka, huzaa bila matatizo yoyote. Watoto wao wachanga huwatembeza kama kundi; na watoto wao hucheza ngoma; hucheza muziki wa ngoma na vinubi, na kufurahia sauti ya filimbi. Huishi maisha ya fanaka kisha hushuka kwa amani kuzimu. Humwambia Mungu, ‘Usitusumbue! Hatutaki kujua matakwa yako. Mungu Mwenye Nguvu ni nini hata tumtumikie? Tunapata faida gani tukimwomba dua?’ Kufanikiwa kwao si kuko mikononi mwao, wakiwa wamemweka Mungu mbali na mipango yao? “Mara ngapi umepata kuona mwanga wa maisha ya mwovu umezimwa, wakapata kukumbwa na maafa, au Mungu amewahi kuwaangamiza kwa hasira yake? Hata hivyo, na wapeperushwe kama majani makavu, wawe kama makapi yanayochukuliwa na dhoruba! “Nyinyi mwasema, ‘Mungu amewawekea watoto wao adhabu ya watu hao waovu.’ Kwa nini hawalipizi wao wenyewe, wapate kutambua! Waone wao wenyewe wakiangamia; waone wenyewe ghadhabu ya Mungu mwenye nguvu. Maana wakifa watajali nini juu ya wazawa wao, wakati siku zao zitakapokuwa zimefika mwisho?

Shirikisha
Soma Yobu 21

Yobu 21:1-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, Yasikizeni sana maneno yangu; Jambo hili na liwe faraja yenu. Niacheni, nami pia nitanena; Tena nikiisha nena, zidini kudhihaki. Mimi, je! Mashitaka yangu yamhusu mwanadamu? Nami kwa nini nisikose kusubiri? Niangalieni, mkastaajabu, Mkaweke mkono kinywani. Hata nikumbukapo nahuzunika, Na utisho wanishika mwilini mwangu. Mbona waovu wanaishi, Na kuwa wazee, naam, na kuongezeka kuwa na nguvu? Kizazi chao kinathibitika nao machoni pao, Na wazao wao mbele ya macho yao. Nyumba zao ni salama bila hofu, Wala fimbo ya Mungu haiwapigi. Fahali wao huvyaza wala hapungukiwi na nguvu; Ng'ombe wao jike huzaa, asiharibu mimba. Huwatoa kama kundi watoto wao. Na watoto wao hucheza. Huimba kwa matari na kwa kinubi, Na kuifurahia sauti ya filimbi. Siku zao hutumia katika kufanikiwa, Kisha hushuka kuzimuni ghafla. Walakini walimwambia Mungu. Tuondokee; Kwani hatutaki kuzijua njia zako. Huyo Mwenyezi ni nani, hata tumtumikie? Nasi tutafaidiwa nini tukimwomba? Tazama, kufanikiwa kwao hakumo mkononi mwao; Mipango ya waovu na iwe mbali nami. Je! Ni mara ngapi taa yao waovu huzimwa? Na msiba wao kuwajia? Na Mungu kuwagawanyia uchungu kwa hasira yake? Ili wawe kama mabua makavu mbele ya upepo, Kama makapi yaliyochukuliwa na dhoruba? Mwasema, Mungu huwawekea watoto wa mtu huo uovu wake. Na amlipe mwenyewe, ili apate kuujua. Macho yake mwenyewe na yaone uharibifu wake, Akanywe ghadhabu zake Mwenyezi. Kwani ana furaha gani katika ukoo wake baada yake, Hesabu ya miezi yake itakapokwisha katwa katikati?

Shirikisha
Soma Yobu 21

Yobu 21:1-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, Yasikizeni sana maneno yangu; Jambo hili na liwe faraja yenu. Niacheni, nami pia nitanena; Tena nikiisha nena, zidini kudhihaki. Mimi, je! Mashitaka yangu yamhusu mwanadamu? Nami kwa nini nisikose kusubiri? Niangalieni, mkastaajabu, Mkaweke mkono kinywani. Hata nikumbukapo nahuzunika, Na utisho wanishika mwilini mwangu. Mbona waovu wanaishi, Na kuwa wazee, naam, na kuongezeka kuwa na nguvu? Kizazi chao kinathibitika nao machoni pao, Na wazao wao mbele ya macho yao. Nyumba zao zi salama pasina hofu, Wala fimbo ya Mungu haiwapigi. Fahali wao huvyaza wala hapungukiwi na nguvu; Ng’ombe wao mke huzaa, asiharibu mimba. Huwatoa kama kundi watoto wao. Na watoto wao hucheza. Huimba kwa matari na kwa kinubi, Na kuifurahia sauti ya filimbi. Siku zao hutumia katika kufanikiwa, Kisha hushuka kuzimuni ghafula. Walakini walimwambia Mungu. Tuondokee; Kwani hatutaki kuzijua njia zako. Huyo Mwenyezi ni nani, hata tumtumikie? Nasi tutafaidiwa nini tukimwomba? Tazama, kufanikiwa kwao hakumo mkononi mwao; Mashauri ya waovu na yawe mbali nami. Je! Ni mara ngapi taa yao waovu huzimishwa? Na msiba wao kuwajilia? Na Mungu kuwagawanyia uchungu kwa hasira yake? Ili wawe kama mabua makavu mbele ya upepo, Kama makapi yaliyochukuliwa na dhoruba? Mwasema, Mungu huwawekea watoto wa mtu huo uovu wake. Na amlipe mwenyewe, ili apate kuujua. Macho yake mwenyewe na yaone uharibifu wake, Akanywe ghadhabu zake Mwenyezi. Kwani ana furaha gani katika mbari yake baada yake, Hesabu ya miezi yake itakapokwisha katwa katikati?

Shirikisha
Soma Yobu 21

Yobu 21:1-21 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Ndipo Ayubu akajibu: “Yasikilizeni maneno yangu kwa makini; hii na iwe faraja mnayonipa mimi. Nivumilieni ninapozungumza, nami nikishazungumza, endeleeni kunidhihaki. “Je, kwani malalamiko yangu yanaelekezwa kwa mwanadamu? Kwa nini nisikose subira? Niangalieni mkastaajabu; mkaweke mkono juu ya vinywa vyenu. Ninapowaza kuhusu hili, ninaogopa, nao mwili wangu unatetemeka. Kwa nini waovu wanaendelea kuishi, wakifikia umri wa uzee na kuendelea kuwa na nguvu? Huwaona watoto wao wakithibitika wakiwa wamewazunguka, wazao wao mbele za macho yao. Nyumba zao zi salama wala hakuna hofu; fimbo ya Mungu haiko juu yao. Madume yao ya ngʼombe huvyaza bila kushindwa kamwe; ngʼombe wao huzaa wala hawaharibu mimba. Huwatoa watoto wao nje kama kundi; wadogo wao huchezacheza. Huimba nyimbo kwa matari na kwa kinubi, nao huifurahia sauti ya filimbi. Huitumia miaka yao katika mafanikio nao hushuka kaburini kwa amani. Lakini humwambia Mungu, ‘Tuache sisi!’ Hatuna haja ya kufahamu njia zako. Mwenyezi ni nani hata tumtumikie? Tutapata faida gani kumwomba? Lakini kufanikiwa kwao hakupo mikononi mwao wenyewe, hivyo najitenga mbali na ushauri wa waovu. “Lakini ni mara ngapi taa ya waovu huzimwa? Ni mara ngapi maafa huwajia, yale yawapatayo ambayo Mungu huwapangia katika hasira yake? Ni mara ngapi huwa kama majani makavu mbele ya upepo, kama makapi yachukuliwayo na dhoruba? Imesemekana, ‘Mungu huiweka akiba adhabu ya mtu kwa ajili ya wanawe.’ Mungu na amlipe mtu mwenyewe, ili apate kulijua! Macho yake mwenyewe na yaone maangamizi yake; yeye na ainywe ghadhabu ya Mwenyezi. Kwani anajali nini kuhusu jamaa anayoiacha nyuma, miezi yake aliyopangiwa ifikapo mwisho?

Shirikisha
Soma Yobu 21