Yobu 15:6-8
Yobu 15:6-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Maneno yako mwenyewe yanakuhukumu, sio mimi; matamshi yako yashuhudia dhidi yako. Je, wewe ni mtu wa kwanza kuzaliwa? Je, wewe ulizaliwa kabla ya kuweko vilima? Je, ulipata kuweko katika halmashauri ya Mungu? au, wewe ndiwe peke yako mwenye hekima?
Yobu 15:6-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kinywa chako mwenyewe chakuhukumia makosa, wala si mimi; Naam, midomo yako mwenyewe hushuhudia juu yako. Je! Wewe u mtu wa kwanza aliyezaliwa? Au, ulizawa wewe kabla ya milima? Je! Umesikiza ushauri wa siri ya Mungu? Nawe je! Wazuia hekima iwe yako tu?
Yobu 15:6-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kinywa chako mwenyewe chakuhukumia makosa, wala si mimi; Naam, midomo yako mwenyewe hushuhudia juu yako. Je! Wewe u mtu wa kwanza aliyezaliwa? Au, ulizawa wewe kabla ya milima? Je! Umesikia mashauri ya siri ya Mungu? Nawe je! Wazuia hekima iwe yako tu?
Yobu 15:6-8 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kinywa chako mwenyewe kinakuhukumu, wala si changu; midomo yako mwenyewe inashuhudia dhidi yako. “Je, wewe ni mtu wa kwanza kuzaliwa? Ulizaliwa kabla ya vilima? Je, wewe husikiliza mashauri ya siri ya Mungu? Je, wewe unaizuia hekima iwe yako mwenyewe?