Yobu 14:7-12
Yobu 14:7-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Maana mti ukikatwa lipo tumaini la kuota, waweza kuchipua tena. Japo mizizi yake itazeeka udongoni, na shina lake kufia ardhini, lakini kwa harufu tu ya maji utachipua; utatoa matawi kama chipukizi. Lakini mtu hufa na huo ndio mwisho wake. Akisha toa roho anabakiwa na nini tena? “Kama vile maji yakaukavyo ziwani, na mto unavyokoma kutiririka, ndivyo anavyokufa mtu, wala haamki tena; hataamka tena wala kugutuka, hata hapo mbingu zitakapotoweka.
Yobu 14:7-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena, Wala machipukizi yake hayatakoma. Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani, Na shina lake kufa katika udongo; Lakini kwa harufu ya maji utachipuka, Na kutoa matawi kama mche. Lakini mwanadamu hufa, hufariki dunia; Naam, mwanadamu hukata roho, naye yupo wapi? Kama vile maji kupwa katika bahari, Na mto kupunguka na kukatika; Ndivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke; Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka, Wala kuamshwa usingizini.
Yobu 14:7-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena, Wala machipukizi yake hayatakoma. Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani, Na shina lake kufa katika udongo; Lakini kwa harufu ya maji utachipuka, Na kutoa matawi kama mche. Lakini mwanadamu hufa, huifariki dunia; Naam, mwanadamu hutoa roho, naye yupo wapi? Kama vile maji kupwa katika bahari, Na mto kupunguka na kukatika; Ni vivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke; Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka, Wala kuamshwa usingizini.
Yobu 14:7-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Kwa maana lipo tumaini kwa mti; kama ukikatwa utachipuka tena, nayo machipukizi yake mapya hayatakoma. Mizizi yake yaweza kuchakaa ardhini na kisiki chake kufa udongoni, lakini kwa kupata dalili ya maji utachipua na kutoa machipukizi kama mche. Lakini mwanadamu hufa, na huo ndio mwisho wake; hutoa pumzi ya mwisho, naye hayuko tena! Kama vile maji yanavyotoweka katika bahari, au mkondo wa mto ukaushwavyo na kuwa mkavu, ndivyo mwanadamu alalavyo chini asiamke; hadi mbingu zitakapokuwa hazipo tena, wanadamu hawataamka au kuamshwa kutoka usingizi wao.