Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yobu 14:1-17

Yobu 14:1-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe. Nawe, je! Wafumbua macho yako kumwangalia mtu kama yeye, Na kunitia katika hukumu pamoja nawe? Ni nani awezaye kutoa kitu kilicho safi kitoke katika kitu kichafu? Hapana awezaye. Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe, Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita; Acha kumwangalia yeye, apate kupumzika, Hata atakapoitimiza siku yake, kama aliyeajiriwa. Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena, Wala machipukizi yake hayatakoma. Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani, Na shina lake kufa katika udongo; Lakini kwa harufu ya maji utachipuka, Na kutoa matawi kama mche. Lakini mwanadamu hufa, hufariki dunia; Naam, mwanadamu hukata roho, naye yupo wapi? Kama vile maji kupwa katika bahari, Na mto kupunguka na kukatika; Ndivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke; Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka, Wala kuamshwa usingizini. Laiti ungenificha kuzimuni, Ukanilinda kwa siri, hata ghadhabu zako zitakapopita, Na kuniandikia muda ulioamriwa, na kunikumbuka! Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena? Mimi ningengoja siku zote za huduma yangu, Hadi kufunguliwa kwangu kunifikie. Wewe ungeita, nami ningekujibu; Ungekuwa na tamaa ya kazi ya mikono yako. Lakini sasa wazihesabu hatua zangu; Je! Huchungulii dhambi yangu? Kosa langu limetiwa mhuri mfukoni, Nawe waufunga uovu wangu.

Shirikisha
Soma Yobu 14

Yobu 14:1-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe. Nawe, je! Wafumbua macho yako kumwangalia mtu kama yeye, Na kunitia katika hukumu pamoja nawe? Ni nani awezaye kutoa kitu kilicho safi kitoke katika kitu kichafu? Hapana awezaye. Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe, Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita; Acha kumwangalia yeye, apate kupumzika, Hata atakapoitimiza siku yake, kama aliyeajiriwa. Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena, Wala machipukizi yake hayatakoma. Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani, Na shina lake kufa katika udongo; Lakini kwa harufu ya maji utachipuka, Na kutoa matawi kama mche. Lakini mwanadamu hufa, huifariki dunia; Naam, mwanadamu hutoa roho, naye yupo wapi? Kama vile maji kupwa katika bahari, Na mto kupunguka na kukatika; Ni vivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke; Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka, Wala kuamshwa usingizini. Laiti ungenificha kuzimuni, Ukanilinda kwa siri, hata ghadhabu zako zitakapopita, Na kuniandikia muda ulioamriwa, na kunikumbuka! Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena? Mimi ningengoja siku zote za vita vyangu, Hata kufunguliwa kwangu kunifikilie. Wewe ungeita, nami ningekujibu; Ungekuwa na tamaa ya kazi ya mikono yako. Lakini sasa wazihesabu hatua zangu; Je! Huchungulii dhambi yangu? Kosa langu limetiwa muhuri mfukoni, Nawe waufunga uovu wangu.

Shirikisha
Soma Yobu 14

Yobu 14:1-17 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

“Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake ni chache nazo zimejaa taabu. Huchanua kama ua kisha hunyauka; huwa kama kivuli kipitacho upesi, wala hadumu. Je, unamwekea jicho lako mtu kama huyo? Je, utamleta mbele yako katika hukumu? Ni nani awezaye kutoa kitu safi kutoka kitu najisi? Hakuna awezaye! Siku za mwanadamu zimewekewa mpaka; umekwisha kutangaza idadi ya miezi yake na kuweka mpaka ambao hawezi kuuvuka. Hivyo angalia mbali umwache, hadi awe amekamilisha muda wake kama mtu aliyeajiriwa. “Kwa maana lipo tumaini kwa mti; kama ukikatwa utachipuka tena, nayo machipukizi yake mapya hayatakoma. Mizizi yake yaweza kuchakaa ardhini na kisiki chake kufa udongoni, lakini kwa kupata dalili ya maji utachipua na kutoa machipukizi kama mche. Lakini mwanadamu hufa, na huo ndio mwisho wake; hutoa pumzi ya mwisho, naye hayuko tena! Kama vile maji yanavyotoweka katika bahari, au mkondo wa mto ukaushwavyo na kuwa mkavu, ndivyo mwanadamu alalavyo chini asiamke; hadi mbingu zitakapokuwa hazipo tena, wanadamu hawataamka au kuamshwa kutoka usingizi wao. “Laiti kama ungenificha kaburini, na kunisitiri hadi hasira yako ipite! Laiti ungeniwekea wakati, na kisha ukanikumbuka! Je, kama mtu akifa, aweza kuishi tena? Siku zote za kazi zangu ngumu nitangojea kufanywa upya kwangu. Utaniita nami nitakuitika; utakionea shauku kiumbe ambacho mikono yako ilikiumba. Hakika ndipo utakapozihesabu hatua zangu, lakini hutazifuatia dhambi zangu. Makosa yangu yatatiwa muhuri kwenye mfuko, nawe utazifunika dhambi zangu.

Shirikisha
Soma Yobu 14