Yobu 13:5-12
Yobu 13:5-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Laiti mngekaa kimya kabisa, ikafikiriwa kwamba mna hekima! Sikilizeni basi hoja yangu, nisikilizeni ninapojitetea. Je, mnadhani mwamtumikia Mungu kwa kusema uongo? Mnafikiri kusema kwa hila kunamfaa yeye? Je, mnajaribu kumpendelea Mungu? Je, mtamtetea Mungu mahakamani? Je, akiwakagua nyinyi mtapona? Au mnadhani mnaweza kumdanganya Mungu kama watu? Hakika yeye atawakemea kama mkionesha upendeleo kwa siri. Je, fahari yake haiwatishi? Je, hampatwi na hofu juu yake? Misemo yenu ni methali za majivu, hoja zenu ni ngome za udongo.
Yobu 13:5-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Laiti mngenyamaza kabisa! Hilo lingekuwa hekima kwenu. Sikieni sasa basi hoja zangu, Mkayasikie malalamiko ya midomo yangu. Je! Mtanena yasiyo ya haki kwa ajili ya Mungu, Na kusema kwa udanganyifu kwa ajili yake? Je! Mtamwonesha yeye upendeleo? Mtamtetea Mungu? Je! Itafaa yeye kuwatafuta ninyi? Au, kama kumdanganya mtu, je! Mtamdanganya yeye? Hakika atawakemea ninyi, Mkiwapendelea watu kwa siri. Je! Huo ukuu wake hautawatia hofu, Na utisho wake hautawaangukia? Maneno yenu ya hekima ni mithali ya majivu, Ngome zenu ni ngome za udongo.
Yobu 13:5-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Laiti mngenyamaza kabisa! Hilo lingekuwa hekima kwenu. Sikieni sasa basi hoja zangu, Mkayasikie mashindano ya midomo yangu. Je! Mtanena yasiyo ya haki kwa ajili ya Mungu, Na kusema kwa udanganyifu kwa ajili yake? Je! Mtamwonyesha yeye upendeleo? Mtamtetea Mungu? Je! Itafaa yeye kuwatafuta ninyi? Au, kama kumdanganya mtu, je! Mtamdanganya yeye? Hakika atawakemea ninyi, Mkiwapendelea watu kwa siri. Je! Huo ukuu wake hautawatia hofu, Na utisho wake hautawaangukia? Matamko yenu ya hekima ni mithali ya majivu, Ngome zenu ni ngome za udongo.
Yobu 13:5-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Laiti wote mngenyamaza! Kwa kuwa kwenu hilo lingekuwa hekima. Sikieni sasa hoja yangu; sikilizeni kusihi kwangu. Je, mtazungumza kwa uovu kwa niaba ya Mungu? Je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa niaba yake? Mtamwonesha upendeleo? Mtamtetea Mungu kwenye mashtaka yake? Je, ingekuwa vyema Mungu akiwahoji ninyi? Je, mngeweza kumdanganya kama ambavyo mngeweza kuwadanganya wanadamu? Hakika angewakemea mkiwapendelea watu kwa siri. Je, huo ukuu wake haungewatisha ninyi? Je, hofu yake isingewaangukia ninyi? Maneno yenu ni mithali za majivu; utetezi wenu ni ngome za udongo wa mfinyanzi.