Yobu 11:13-18
Yobu 11:13-18 Biblia Habari Njema (BHN)
“Yobu, ukiufanya moyo wako mnyofu, utainua mikono yako kumwomba Mungu! Kama una uovu, utupilie mbali. Usikubali ubaya uwemo nyumbani mwako. Hapo utajitokeza mbele ya watu bila lawama, utakuwa thabiti bila kuwa na hofu. Utazisahau taabu zako zote; utazikumbuka tu kama mafuriko yaliyopita. Maisha yako yatangaa kuliko jua la adhuhuri, giza lake litabadilika kuwa mngao wa pambazuko. Utakuwa na ujasiri maana lipo tumaini; utalindwa na kupumzika salama.
Yobu 11:13-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wewe ukiuweka moyo wako kwa uelekevu, Na kumnyoshea mikono yako; Ikiwa una uovu mkononi mwako, uweke mbali nawe, Wala usikubali upuzi kukaa hemani mwako; Hakika ndipo utakapopata kuinua uso pasipo ila; Naam, utathibitika, wala hutakuwa na hofu; Kwa kuwa utasahau mateso yako; Utayakumbuka kama maji yaliyokwisha pita; Na maisha yako yatakuwa meupe kuliko adhuhuri; Giza lake litakuwa kama alfajiri. Nawe utakuwa salama, kwa sababu kuna matumaini; Naam, utatafutatafuta kando yako, na kupumzika salama.
Yobu 11:13-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wewe ukiuweka moyo wako kwa uelekevu, Na kumnyoshea mikono yako; Ikiwa una uovu mkononi mwako, uweke mbali nawe, Wala usikubali upuzi kukaa hemani mwako; Hakika ndipo utakapopata kuinua uso pasipo ila; Naam, utathibitika, wala hutakuwa na hofu; Kwa kuwa utasahau mashaka yako; Utayakumbuka kama maji yaliyokwisha pita; Na maisha yako yatakuwa meupe kuliko adhuhuri; Lijapokuwa ni giza, litakuwa kama alfajiri. Nawe utakuwa salama, kwa sababu kuna matumaini; Naam, utatafuta-tafuta kando yako, na kupumzika katika salama.
Yobu 11:13-18 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Hata sasa ukiutoa moyo wako kwake na kumwinulia mikono yako, ukiiondolea mbali ile dhambi iliyo mkononi mwako, wala usiuruhusu uovu ukae kwenye hema lako, ndipo utainua uso wako bila aibu; utasimama imara bila hofu. Hakika utaisahau taabu yako, utaikumbuka tu kama maji yaliyokwisha kupita. Maisha yako yatangʼaa kuliko adhuhuri, nalo giza litakuwa kama alfajiri. Utakuwa salama, kwa kuwa lipo tumaini; utatazama pande zote na kupumzika kwa salama.