Yohane 5:41-44
Yohane 5:41-44 Biblia Habari Njema (BHN)
“Shabaha yangu si kupata sifa kutoka kwa watu. Lakini nawajua nyinyi, najua kwamba upendo kwa Mungu haumo mioyoni mwenu. Mimi nimekuja kwa mamlaka ya Baba yangu, lakini hamnipokei; bali mtu mwingine akija kwa mamlaka yake mwenyewe, mtampokea. Mwawezaje kuamini, hali nyinyi mnapenda kupokea sifa kutoka kwenu nyinyi wenyewe, wala hamtafuti sifa kutoka kwake yeye aliye peke yake Mungu?
Yohane 5:41-44 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mimi siupokei utukufu kwa wanadamu. Lakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu. Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo. Mnawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?
Yohane 5:41-44 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mimi siupokei utukufu kwa wanadamu. Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu. Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo. Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?
Yohane 5:41-44 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Mimi sikubali kutukuzwa na wanadamu, lakini mimi ninawafahamu. Ninajua kwamba hamna upendo wa Mungu mioyoni mwenu. Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, nanyi hamnipokei. Lakini mtu mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea. Mnawezaje kuamini ikiwa mnapeana utukufu ninyi kwa ninyi, lakini hamfanyi bidii kupata utukufu unaotoka kwa Mungu?