Yohane 21:24-25
Yohane 21:24-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Huyo ndiye yule aliyeshuhudia mambo haya na kuyaandika. Nasi twajua kwamba aliyoyasema ni kweli. Kuna mambo mengine mengi aliyofanya Yesu, ambayo kama yangeandikwa yote, moja baada ya lingine, nadhani hata ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.
Yohane 21:24-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Huyu ndiye yule mwanafunzi ayashuhudiaye haya, na aliyeyaandika haya: nasi twajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli. Pia kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.
Yohane 21:24-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Huyu ndiye yule mwanafunzi ayashuhudiaye haya, na aliyeyaandika haya: nasi twajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli. Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.
Yohane 21:24-25 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Huyu ndiye yule mwanafunzi anayeshuhudia mambo haya, na ndiye ameandika habari hizi. Nasi tunajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli. Lakini kuna mambo mengine mengi ambayo Yesu alifanya. Kama yote yangeandikwa, nadhani hata ulimwengu wote haungekuwa na nafasi ya kutosha kuweka vitabu ambavyo vingeandikwa.