Yohane 2:7-9
Yohane 2:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Yesu akawaambia, “Ijazeni mitungi hiyo maji.” Nao wakaijaza mpaka juu. Kisha akawaambia, “Sasa choteni mkampelekee mkuu wa karamu.” Mkuu wa karamu alipoonja hayo maji, kumbe yalikuwa yamegeuka kuwa divai. Yeye hakujua ilikotoka, (lakini wale watumishi waliochota maji walijua). Mkuu wa karamu akamwita bwana arusi
Yohane 2:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza mpaka juu. Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa sherehe. Wakapeleka. Naye mkuu wa sherehe alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa sherehe alimwita bwana arusi
Yohane 2:7-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu. Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka. Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi
Yohane 2:7-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Yesu akawaambia wale watumishi, “Ijazeni hiyo mitungi maji.” Nao wakaijaza ile mitungi hadi juu. Kisha akawaambia, “Sasa choteni hayo maji kidogo; mpelekeeni mkuu wa sherehe.” Hivyo wakachota, wakampelekea. Yule mkuu wa sherehe akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yamebadilishwa kuwa divai. Hakujua divai hiyo ilikotoka ingawa wale watumishi waliochota yale maji walifahamu. Basi akamwita bwana arusi kando