Yohane 16:12-13
Yohane 16:12-13 Biblia Habari Njema (BHN)
“Ninayo bado mengi ya kuwaambieni, ila kwa sasa hamwezi kuyastahimili. Lakini atakapokuja huyo Roho wa ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote; maana hatasema kwa mamlaka yake mwenyewe, bali atasema atakayoyasikia na kuwajulisheni yatakayokuja.
Yohane 16:12-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hata bado ningali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamuwezi kuyastahimili hivi sasa. Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Yohane 16:12-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Yohane 16:12-13 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Bado ninayo mambo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili sasa. Atakapokuja huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye hatanena kwa ajili yake mwenyewe, bali atanena yale yote atakayosikia, naye atawaonesha mambo yajayo.