Yohane 14:2-4
Yohane 14:2-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama isingekuwa hivyo, ningalikwisha waambieni. Sasa nakwenda kuwatayarishieni nafasi. Na nikienda na kuwatayarishieni nafasi, nitarudi na kuwachukueni kwangu, ili nanyi muwe pale nilipo mimi. Mnajua njia ya kwenda huko ninakokwenda.”
Yohane 14:2-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo. Nami niendako mwaijua njia.
Yohane 14:2-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. Nami niendako mwaijua njia.
Yohane 14:2-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nyumbani mwa Baba yangu kuna makao mengi. Kama sivyo, ningewaambia. Naenda kuwaandalia makao. Nami nikienda na kuwaandalia makao, nitarudi tena na kuwachukua mkae pamoja nami, ili mahali nilipo nanyi mpate kuwepo. Ninyi mnajua njia ya kufika ninakoenda.”