Yeremia 9:3-9
Yeremia 9:3-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Hupinda maneno yao kama pinde; wameimarika kwa uongo na si kwa haki. Huendelea kutoka uovu hata uovu, wala hawanitambui mimi. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Kila mmoja ajihadhari na jirani yake! Hata ndugu yeyote haaminiki, kila ndugu ni mdanganyifu, na kila jirani ni msengenyaji. Kila mmoja humdanganya jirani yake, hakuna hata mmoja asemaye ukweli. Wamezifundisha ndimi zao kusema uongo; hutenda uovu kiasi cha kushindwa kabisa kutubu. Wanarundika dhuluma juu ya dhuluma, na udanganyifu juu ya udanganyifu. Wanakataa kunitambua mimi. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema: Tazama, nitawayeyusha na kuwajaribu! Au, nifanye nini zaidi na watu wangu waovu? Ndimi zao ni kama mishale yenye sumu, daima haziishi kudanganya; kila mmoja huongea vema na jirani yake, lakini moyoni mwake hupanga kumshambulia. Je, nisiwaadhibu kwa sababu ya mambo haya? Je, nisilipe kisasi kwa taifa kama hili? Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Yeremia 9:3-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Huupinda ulimi wao, kana kwamba ni upinde, ili kusema uongo; nao wamepata nguvu katika nchi, lakini si katika uaminifu; maana huendelea toka ubaya hata ubaya, wala hawanijui mimi, asema BWANA. Jihadharini, kila mtu na jirani yake, wala msimtumaini ndugu awaye yote; maana kila ndugu atachongea, na kila jirani atakwenda huku na huko na kusingizia. Nao watadanganya kila mtu jirani yake, wala hawatasema kweli; wameuzoesha ulimi wao kusema uongo; hujidhoofisha ili kutenda uovu. Makao yako ya katikati ya hadaa; kwa hadaa wanakataa kunijua mimi, asema BWANA. Basi, kwa hiyo BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawayeyusha na kuwajaribu; maana nisipotenda hivi, nitende nini kwa ajili ya binti ya watu wangu? Ulimi wao ni mshale ufishao; husema maneno ya hadaa; mtu mmoja husema maneno ya amani na mwenzake kwa kinywa chake, lakini moyoni mwake humwotea. Je! Nisiwaadhibu kwa mambo hayo? Asema BWANA; na nafsi yangu je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna hii?
Yeremia 9:3-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Huupinda ulimi wao, kana kwamba ni upinde, ili kusema uongo; nao wamepata nguvu katika nchi, lakini si katika uaminifu; maana huendelea toka ubaya hata ubaya, wala hawanijui mimi, asema BWANA. Jihadharini, kila mtu na jirani yake, wala msimtumaini ndugu awaye yote; maana kila ndugu atachongea, na kila jirani atakwenda huko na huko na kusingizia. Nao watadanganya kila mtu jirani yake, wala hawatasema kweli; wameuzoeza ulimi wao kusema uongo; hujidhoofisha ili kutenda uovu. Makao yako ya katikati ya hadaa; kwa hadaa wanakataa kunijua mimi, asema BWANA. Basi, kwa hiyo BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawayeyusha na kuwajaribu; maana nisipotenda hivi, nitende nini kwa ajili ya binti ya watu wangu? Ulimi wao ni mshale ufishao; husema maneno ya hadaa; mtu mmoja husema maneno ya amani na mwenzake kwa kinywa chake, lakini moyoni mwake humwotea. Je! Nisiwapatilize kwa mambo hayo? Asema BWANA; na nafsi yangu je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna hii?
Yeremia 9:3-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Huweka tayari ndimi zao kama upinde, ili kurusha uongo; wamekuwa na nguvu katika nchi lakini si katika ukweli. Wanatoka dhambi moja hadi nyingine, hawanitambui mimi,” asema BWANA. “Jihadhari na rafiki zako; usiwaamini ndugu zako. Kwa kuwa kila ndugu ni mdanganyifu, na kila rafiki ni msingiziaji. Rafiki humdanganya rafiki, hakuna yeyote asemaye kweli. Wamefundisha ndimi zao kudanganya, wanajichosha wenyewe katika kutenda dhambi. Unakaa katikati ya udanganyifu; katika udanganyifu wao wanakataa kunitambua mimi,” asema BWANA. Kwa hiyo hili ndilo asemalo BWANA wa majeshi: “Tazama, nitawasafisha na kuwajaribu, kwani ni nini kingine niwezacho kufanya kwa sababu ya dhambi ya watu wangu? Ndimi zao ni mshale wenye sumu, hunena kwa udanganyifu. Kwa kinywa chake kila mmoja huzungumza maneno mazuri na jirani yake, lakini moyoni mwake humtegea mtego. Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya jambo hili?” asema BWANA. “Je, nisijilipizie kisasi kwa taifa kama hili?”