Yeremia 9:25-26
Yeremia 9:25-26 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu asema: “Siku zaja ambapo nitawaadhibu wote waliotahiriwa mwilini tu: Wamisri, Wayuda, Waedomu, Waamoni, Wamoabu na wakazi wote wa jangwani wanaonyoa denge. Maana watu hawa wote na Waisraeli wote hawakutahiriwa moyoni.”
Yeremia 9:25-26 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tazama, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapowaadhibu wote waliotahiriwa katika hali yao ya kutotahiriwa; Misri, na Yuda, na Edomu, na wana wa Amoni, na Moabu, na wote wenye kunyoa denge, wakaao nyikani; maana mataifa hayo yote hawana tohara, wala nyumba yote ya Israeli hawakutahiriwa mioyo yao.
Yeremia 9:25-26 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tazama, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapowaadhibu wote waliotahiriwa katika hali yao ya kutokutahiriwa; Misri, na Yuda, na Edomu, na wana wa Amoni, na Moabu, na wote wenye kunyoa denge, wakaao nyikani; maana mataifa hayo yote hawana tohara, wala nyumba yote ya Israeli hawakutahiriwa mioyo yao.
Yeremia 9:25-26 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Siku zinakuja, nitakapowaadhibu wale wote ambao wametahiriwa kimwili tu, asema BWANA, yaani Misri, Yuda, Edomu, Amoni, Moabu na wote wanaoishi jangwani sehemu za mbali. Kwa maana mataifa haya yote hayakutahiriwa mioyo yao, nayo nyumba yote ya Israeli haikutahiriwa.”