Yeremia 8:4-7
Yeremia 8:4-7 Biblia Habari Njema (BHN)
“Wewe Yeremia utawaambia kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Mtu akianguka, je hainuki tena? Mtu akipotea, je, hairudii tena njia yake? Mbona basi, watu hawa wameacha njia iliyo sawa na kuendelea katika upotovu wao? Wanashikilia miungu yao ya uongo, na kukataa kunirudia mimi! Mimi nilisikiliza kwa makini, lakini wao hawakusema ukweli wowote. Hakuna mtu anayetubu uovu wake, wala kujiuliza; ‘Nimefanya nini?’ Kila mmoja wao anashika njia yake, kama farasi akimbiliavyo moja kwa moja vitani. Hata korongo anajua wakati wa kuhama; njiwa, mbayuwayu na koikoi, hufuata majira yao ya kurudi. Lakini watu wangu hawa hawajui kitu juu ya amri zangu mimi Mwenyezi-Mungu.
Yeremia 8:4-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tena utawaambia, BWANA asema hivi, Je! Watu wataanguka, wasisimame tena? Je! Mtu atageuka aende zake, asirudi tena? Mbona, basi, watu hawa wa Yerusalemu wamegeuka waende nyuma, wasikome kugeuka hivyo? Hushika udanganyifu sana, hukataa kurudi. Nilisikiliza nikasikia, lakini walisema yasiyo sawa; hapana mtu aliyetubia maovu yake, akisema, Nimefanya nini? Kila mtu hurudia mwendo wake mwenyewe, kama farasi aendavyo kasi vitani. Naam, koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui amri za BWANA.
Yeremia 8:4-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tena utawaambia, BWANA asema hivi, Je! Watu wataanguka, wasisimame tena? Je! Mtu atageuka aende zake, asirudi tena? Mbona, basi, watu hawa wa Yerusalemu wamegeuka waende nyuma, wasikome kugeuka hivyo? Hushika udanganyifu sana, hukataa kurudi. Nalisikiliza nikasikia, lakini walisema yasiyo sawa; hapana mtu aliyetubia maovu yake, akisema, Nimefanya nini? Kila mtu hurudia mwendo wake mwenyewe, kama farasi aendavyo kasi vitani. Naam, koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui amri za BWANA.
Yeremia 8:4-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Waambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo BWANA: “ ‘Je, watu wanapoanguka hawainuki? Je, mtu anapopotea harudi? Kwa nini basi watu hawa waliasi? Kwa nini Yerusalemu wanaasi kila mara? Wanangʼangʼania udanganyifu na wanakataa kurudi. Nimewasikiliza kwa makini, lakini hawataki kusema lililo sawa. Hakuna anayetubu makosa yake akisema, “Nimefanya nini?” Kila mmoja hufuata njia yake mwenyewe kama farasi anayeenda vitani. Hata korongo aliye angani anayajua majira yake yaliyoamriwa, nao njiwa, mbayuwayu na koikoi hufuata majira yao ya kurudi. Lakini watu wangu hawajui BWANA anachotaka kwao.