Yeremia 52:4
Yeremia 52:4 Biblia Habari Njema (BHN)
Ikawa katika siku ya kumi ya mwezi wa kumi, mwaka wa tisa wa kutawala kwake Sedekia, Nebukadneza mfalme wa Babuloni, alifika na jeshi lake lote kuushambulia Yerusalemu, wakauzingira kila upande.
Yeremia 52:4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikawa, katika mwaka wa tisa wa kumiliki kwake, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, akaja, yeye na jeshi lake lote, juu ya Yerusalemu, akapanga hema zake juu yake; nao wakajenga ngome juu yake pande zote.
Yeremia 52:4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikawa, katika mwaka wa kenda wa kumiliki kwake, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akaja, yeye na jeshi lake lote, juu ya Yerusalemu, akapanga hema zake juu yake; nao wakajenga ngome juu yake pande zote.
Yeremia 52:4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hivyo katika mwaka wa tisa wa utawala wa Sedekia, katika siku ya kumi ya mwezi wa kumi, Nebukadneza mfalme wa Babeli akiwa na jeshi lake lote alifanya vita dhidi ya Yerusalemu. Wakapiga kambi nje ya mji na kuuzingira pande zote.