Yeremia 5:8-9
Yeremia 5:8-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Walikuwa kama farasi walioshiba wenye tamaa, kila mmoja akimtamani mke wa jirani yake. Je, nisiwaadhibu kwa mambo haya yote? Nisilipize kisasi juu ya taifa kama hili?
Yeremia 5:8-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Walikuwa kama farasi walioshiba wakati wa asubuhi; kila mmoja akalia kwa kutamani mke wa mwenzake. Je! Nisiwapatilize kwa sababu ya mambo hayo? Asema BWANA; na nafsi yangu, je! Nisijilipizie kisasi juu ya taifa la namna hii?
Yeremia 5:8-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Walikuwa kama farasi walioshiba wakati wa asubuhi; kila mmoja akalia kwa kutamani mke wa mwenzake. Je! Nisiwapatilize kwa sababu ya mambo hayo? Asema BWANA; na nafsi yangu, je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna hii?