Yeremia 5:23-24
Yeremia 5:23-24 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini watu hawa wana moyo wa ukaidi na uasi; wameniacha wakaenda zao. Wala hawasemi mioyoni mwao; ‘Na tumche Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, anayetujalia mvua kwa wakati wake, anayetupatia mvua za masika na mvua za vuli; na kutupa majira maalumu ya mavuno.’
Yeremia 5:23-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini watu hawa wana moyo wa kuasi na ukaidi; wameasi, wamekwenda zao. Wala hawasemi mioyoni mwao, Basi, na tumche BWANA, Mungu wetu, aletaye mvua, mvua ya mwaka, na mvua ya vuli, kwa wakati wake; na kutuwekea majuma ya mavuno yaliyoamriwa.
Yeremia 5:23-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini watu hawa wana moyo wa kuasi na ukaidi; wameasi, wamekwenda zao. Wala hawasemi mioyoni mwao, Basi, na tumche BWANA, Mungu wetu, aletaye mvua, mvua ya mwaka, na mvua ya vuli, kwa wakati wake; na kutuwekea juma za mavuno zilizoamriwa.
Yeremia 5:23-24 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini watu hawa wana mioyo ya ukaidi na ya uasi, wamegeukia mbali na kwenda zao. Wao hawaambiani wenyewe, ‘Sisi na tumwogope BWANA Mungu wetu, anayetupatia mvua za masika na za vuli kwa majira yake, anayetuhakikishia majuma ya mavuno kwa utaratibu.’