Yeremia 47:1-2
Yeremia 47:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Neno la Mwenyezi-Mungu lililomjia nabii Yeremia kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajaushambulia mji wa Gaza: Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Tazama! Maji yanapanda kutoka kaskazini, nayo yatakuwa mto uliofurika; yataifunika nchi nzima na vyote vilivyomo, mji na wakazi na wanaoishi humo. Watu watalia, wakazi wote wa nchi wataomboleza.
Yeremia 47:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Neno la BWANA lililomjia Yeremia, nabii, kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajashambulia Gaza. BWANA asema hivi, Tazama, maji yanatokea katika pande za kaskazini, nayo yatakuwa mto ufurikao, nayo yataifunika nchi, na kila kitu kilichomo, huo mji na wote wakaao ndani yake; nao watu watalia na watu wote wakaao katika nchi wataomboleza.
Yeremia 47:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Neno la BWANA lililomjia Yeremia, nabii, katika habari za Wafilisti, kabla Farao hajapiga Gaza. 2:4-7; Zek 9:5-7 BWANA asema hivi, Tazama, maji yanatokea katika pande za kaskazini, nayo yatakuwa mto ufurikao, nayo yataifunika nchi, na kila kitu kilichomo, huo mji na wote wakaao ndani yake; nao watu watalia na watu wote wakaao katika nchi watapiga yowe.
Yeremia 47:1-2 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hili ndilo neno la BWANA lililomjia nabii Yeremia kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajaishambulia Gaza: Hili ndilo asemalo BWANA: “Tazama jinsi maji yanavyoinuka huko kaskazini, yatakuwa mafuriko yenye nguvu sana. Yataifurikia nchi na vitu vyote vilivyo ndani yake, miji na wanaoishi ndani yake. Watu watapiga kelele; wote wanaoishi katika nchi wataomboleza