Yeremia 46:27
Yeremia 46:27 Biblia Habari Njema (BHN)
“Lakini wewe usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, usifadhaike, ee Israeli; maana, kutoka mbali nitakuokoa, nitakuja kuwaokoa wazawa wako kutoka nchi walimohamishwa. Yakobo utarudi na kutulia na kustarehe, wala hakuna yeyote atakayekutia hofu.
Yeremia 46:27 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini usiogope wewe, Ee Yakobo, mtumishi wangu; wala usifadhaike, Ee Israeli; kwa maana, tazama, nitakuokoa toka mbali, na wazao wako toka nchi ya uhamisho wao; na Yakobo atarudi, naye atatulia na kustarehe, wala hapana mtu atakayemtia hofu.
Yeremia 46:27 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini usiogope wewe, Ee Yakobo, mtumishi wangu; wala usifadhaike, Ee Israeli; kwa maana, tazama, nitakuokoa toka mbali, na wazao wako toka nchi ya uhamisho wao; na Yakobo atarudi, naye atatulia na kustarehe, wala hapana mtu atakayemtia hofu.
Yeremia 46:27 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, usifadhaike, ee Israeli. Hakika nitakuokoa kutoka nchi za mbali, uzao wako kutoka nchi walioishi uhamishoni. Yakobo atakuwa tena na amani na salama, wala hakuna hata mmoja atakayewatia hofu.