Yeremia 2:4-5
Yeremia 2:4-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu, enyi wazawa wa Yakobo. Sikilizeni enyi jamaa zote za wazawa wa Israeli. Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wazee wenu waliona kosa gani kwangu hata wakanigeuka na kuniacha, wakakimbilia miungu duni, hata nao wakawa watu duni?
Yeremia 2:4-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lisikieni neno la BWANA, ninyi nyumba ya Yakobo, na ninyi, jamaa zote za nyumba ya Israeli. BWANA asema hivi, Baba zenu waliona dhuluma gani kwangu, hata wakafarakana nami, wakafuata ubatili, nao wakawa ubatili?
Yeremia 2:4-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lisikieni neno la BWANA, ninyi nyumba ya Yakobo, na ninyi, jamaa zote za nyumba ya Israeli. BWANA asema hivi, Baba zenu waliona dhuluma gani kwangu, hata wakafarakana nami, wakafuata ubatili, nao wakawa ubatili?
Yeremia 2:4-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Sikia neno la BWANA, ee nyumba ya Yakobo, nanyi nyote jamaa za nyumba ya Israeli. Hivi ndivyo asemavyo BWANA: “Je, baba zenu waliona kosa gani kwangu, hata wakatangatanga mbali nami hivyo? Walifuata sanamu zisizofaa, nao wenyewe wakawa hawafai.