Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 2:1-13

Yeremia 2:1-13 Biblia Habari Njema (BHN)

Neno la Mwenyezi-Mungu likanijia: “Nenda ukawatangazie waziwazi wakazi wote wa Yerusalemu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Naukumbuka uaminifu wako ulipokuwa kijana, jinsi ulivyonipenda kama mchumba wako, ulivyonifuata jangwani kwenye nchi ambayo haikupandwa kitu. Israeli, wewe ulikuwa mtakatifu kwangu, ulikuwa matunda ya kwanza ya mavuno yangu. Wote waliokudhuru walikuwa na hatia, wakapatwa na maafa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.” Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu, enyi wazawa wa Yakobo. Sikilizeni enyi jamaa zote za wazawa wa Israeli. Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Wazee wenu waliona kosa gani kwangu hata wakanigeuka na kuniacha, wakakimbilia miungu duni, hata nao wakawa watu duni? Hawakujiuliza: ‘Yuko wapi Mwenyezi-Mungu aliyetutoa nchini Misri, aliyetuongoza nyikani katika nchi ya jangwa na makorongo, nchi kame na yenye giza nene, nchi isiyopitiwa na mtu yeyote, wala kukaliwa na binadamu?’ Niliwaleta katika nchi yenye rutuba, muyafurahie mazao yake na mema yake mengine. Lakini mlipofika tu mliichafua nchi yangu, mkaifanya chukizo nchi niliyowapa iwe yenu. Nao makuhani hawakujiuliza: ‘Yuko wapi Mwenyezi-Mungu?’ Wataalamu wa sheria hawakunijua, viongozi wa watu waliniasi; manabii nao walitabiri kwa jina la Baali na kuabudu sanamu zisizo na faida yoyote.” Mwenyezi-Mungu asema, “Kwa hiyo, mimi nitawalaumu nyinyi, na nitawalaumu wazawa wenu. Haya, vukeni bahari hadi Kupro mkaone, au tumeni watu huko Kedari wakachunguze, kama jambo kama hili limewahi kutokea: Kwamba kuna taifa lililowahi kubadilisha miungu yake ingawa miungu hiyo si miungu! Lakini watu wangu wameniacha mimi, utukufu wao, wakafuata miungu isiyofaa kitu. Shangaeni enyi mbingu, juu ya jambo hili, mkastaajabu na kufadhaika kabisa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Maana, watu wangu wametenda maovu mawili; wameniacha mimi niliye chemchemi ya maji ya uhai, wakajichimbia visima vyao wenyewe, visima vyenye nyufa, visivyoweza kuhifadhi maji.

Shirikisha
Soma Yeremia 2

Yeremia 2:1-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Neno la BWANA likanijia, kusema, Nenda ukalie masikioni mwa Yerusalemu, ukisema, BWANA asema hivi, Nakukumbuka, hisani ya ujana wako, upendo wa wakati wa kuposwa kwako; Jinsi ulivyonifuata huko jangwani, katika nchi isiyopandwa mbegu. Israeli walikuwa utakatifu kwa BWANA; malimbuko ya uzao wake; Wote watakaomla watakuwa na hatia; uovu utawajia; asema BWANA. Lisikieni neno la BWANA, ninyi nyumba ya Yakobo, na ninyi, jamaa zote za nyumba ya Israeli. BWANA asema hivi, Baba zenu waliona dhuluma gani kwangu, hata wakafarakana nami, wakafuata ubatili, nao wakawa ubatili? Wala hawakusema, Yuko wapi BWANA, aliyetutoa katika nchi ya Misri; akatuongoza jangwani, katika nchi ya ukame na mashimo, katika nchi ya kiu na ya kivuli cha mauti, katika nchi ambayo ndani yake hapiti mtu, wala haikukaliwa na watu? Nami nikawatia katika nchi ya shibe, mpate kula matunda yake na mema yake; lakini ninyi mlipoingia katika nchi ile, mliitia unajisi nchi yangu, na urithi wangu mliufanya kuwa chukizo. Makuhani hawakusema, Yuko wapi BWANA? Wala wanasheria hawakunijua; wachungaji nao waliniasi, nao manabii walitoa unabii kwa Baali, wakafuata mambo yasiyofaidia kitu. Basi, kwa ajili ya hayo nitateta nanyi, asema BWANA, nami nitateta na watoto wa watoto wenu. Maana, vukeni mpaka visiwa vya Kitimu, mkaone; tumeni watu waende Kedari, mkafikiri sana; mkaone kwamba jambo kama hili limekuwa wakati wowote. Je! Taifa wamebadili miungu yao, ingawa siyo miungu? Lakini watu wangu wameubadili utukufu wao kwa ajili ya kitu kisichofaidia. Enyi mbingu, staajabuni kwa ajili ya jambo hili, mkaogope sana, na kuwa ukiwa sana, asema BWANA. Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia visima, visima vyenye nyufa visivyoweza kuweka maji.

Shirikisha
Soma Yeremia 2

Yeremia 2:1-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Neno la BWANA likanijia, kusema, Enenda ukalie masikioni mwa Yerusalemu, ukisema, BWANA asema hivi, Nakukumbuka, hisani ya ujana wako, upendo wa wakati wa uposo wako; Jinsi ulivyonifuata huko jangwani, katika nchi isiyopandwa mbegu. Israeli walikuwa utakatifu kwa BWANA; malimbuko ya uzao wake; Wote watakaomla watakuwa na hatia; uovu utawajilia; asema BWANA. Lisikieni neno la BWANA, ninyi nyumba ya Yakobo, na ninyi, jamaa zote za nyumba ya Israeli. BWANA asema hivi, Baba zenu waliona dhuluma gani kwangu, hata wakafarakana nami, wakafuata ubatili, nao wakawa ubatili? Wala hawakusema, Yuko wapi BWANA, aliyetutoa katika nchi ya Misri; akatuongoza jangwani, katika nchi ya ukame na mashimo, katika nchi ya kiu na ya kivuli cha mauti, katika nchi ambayo ndani yake hapiti mtu, wala haikukaliwa na watu? Nami nikawatia katika nchi ya shibe, mpate kula matunda yake na mema yake; lakini ninyi mlipoingia katika nchi ile, mliitia unajisi nchi yangu, na urithi wangu mliufanya kuwa chukizo. Makuhani hawakusema, Yuko wapi BWANA? Wala wana-sheria hawakunijua; wachungaji nao waliniasi, nao manabii walitoa unabii kwa Baali, wakafuata mambo yasiyofaidia kitu. Basi, kwa ajili ya hayo nitateta nanyi, asema BWANA, nami nitateta na watoto wa watoto wenu. Maana, vukeni mpaka visiwa vya Kitimu, mkaone; tumeni watu waende Kedari, mkafikiri sana; mkaone kwamba jambo kama hili limekuwa wakati wo wote. Je! Taifa wamebadili miungu yao, ingawa siyo miungu? Lakini watu wangu wameubadili utukufu wao kwa ajili ya kitu kisichofaidia. Enyi mbingu, staajabuni kwa ajili ya jambo hili, mkaogope sana, na kuwa ukiwa sana, asema BWANA. Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia mabirika, mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji.

Shirikisha
Soma Yeremia 2

Yeremia 2:1-13 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Neno la BWANA lilinijia kusema, “Nenda ukahubiri masikioni mwa watu wa Yerusalemu: “Hivi ndivyo asemavyo BWANA: “ ‘Nakumbuka moyo wako wa uchaji katika ujana wako, jinsi ulivyonipenda kama bibi arusi na kunifuata katika jangwa lile lote, katika nchi isiyopandwa mbegu. Israeli alikuwa mtakatifu kwa BWANA, kama malimbuko ya kwanza ya mavuno yake; wote waliomwangamiza walihesabiwa kuwa na hatia, nayo maafa yaliwakumba,’ ” asema BWANA. Sikia neno la BWANA, ee nyumba ya Yakobo, nanyi nyote jamaa za nyumba ya Israeli. Hivi ndivyo asemavyo BWANA: “Je, baba zenu waliona kosa gani kwangu, hata wakatangatanga mbali nami hivyo? Walifuata sanamu batili, nao wenyewe wakawa batili. Hawakuuliza, ‘Yuko wapi BWANA, aliyetupandisha kutoka Misri na kutuongoza kupitia nyika kame, kupitia nchi ya majangwa na mabonde, nchi ya ukame na giza, nchi ambayo hakuna mtu asafiriye ndani yake wala hakuna mtu aishiye humo?’ Niliwaleta katika nchi yenye wingi wa vitu ili mpate kula matunda yake na utajiri wa mazao yake. Lakini mkaja na kuinajisi nchi yangu, na kuufanya urithi wangu chukizo. Makuhani hawakuuliza, ‘Yuko wapi BWANA?’ Wale wanaoshughulikia sheria hawakunijua mimi; viongozi waliasi dhidi yangu. Manabii walitabiri kwa jina la Baali, wakifuata sanamu batili. “Kwa hiyo naleta tena mashtaka dhidi yako,” asema BWANA. “Nami nitaleta mashtaka dhidi ya watoto wa watoto wako. Vuka, nenda ngʼambo hadi pwani ya Kitimu nawe uangalie, tuma watu waende Kedari, wachunguze kwa makini, uone kama kumeshawahi kuwa kitu kama hiki. Je, taifa limebadili miungu yake wakati wowote? (Hata ingawa hao si miungu kamwe.) Lakini watu wangu wamebadili Utukufu wao kwa sanamu batili. Shangaeni katika hili, ee mbingu, nanyi tetemekeni kwa hofu kuu,” asema BWANA. “Watu wangu wametenda dhambi mbili: Wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji yaliyo hai, nao wamejichimbia visima vyao wenyewe, visima vilivyobomoka, visivyoweza kuhifadhi maji.

Shirikisha
Soma Yeremia 2