Yeremia 18:18
Yeremia 18:18 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha, watu wakasema: “Njoni tumfanyie Yeremia njama, maana hatukosi makuhani wa kutufundisha, wenye hekima wa kutushauri na manabii wa kututangazia ujumbe wa Mungu! Njoni tumshtaki kwa maneno yake mwenyewe, wala tusiyatilie maanani yote asemayo.”
Yeremia 18:18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hapo ndipo waliposema, Njooni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njooni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yoyote.
Yeremia 18:18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hapo ndipo waliposema, Njoni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njoni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yo yote.
Yeremia 18:18 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wakasema, “Njooni, tutunge hila dhidi ya Yeremia; kwa kuwa kufundisha sheria kwa kuhani hakutapotea, wala shauri litokalo kwa mwenye hekima, wala neno la manabii. Hivyo njooni, tumshambulie kwa ndimi zetu na tusijali chochote asemacho.”