Yeremia 15:1-4
Yeremia 15:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Hata kama Mose na Samueli wangesimama mbele yangu na kunisihi, nisingewahurumia watu hawa. Waondoe kabisa mbele yangu. Waache waende zao! Na wakikuuliza, ‘Twende wapi?’ wewe utawajibu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Waliopangiwa kufa kwa maradhi, watakufa kwa maradhi; waliopangiwa kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga; waliopangiwa kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa; na waliopangiwa kuwa mateka, watatekwa mateka. Mimi Mwenyezi-Mungu nimeamua kuwaletea aina nne za maangamizi: Vita itakayowaua, mbwa watakaowararua; ndege wa angani watakaowadonoa na wanyama wa porini watakaowatafuna na kuwamaliza. Nitawafanya kuwa kitu cha kutisha kwa falme zote za dunia, kwa sababu ya mambo ambayo Manase mwana wa Hezekia, aliyafanya huko Yerusalemu, alipokuwa mfalme wa Yuda.
Yeremia 15:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo BWANA akaniambia, Hata wangesimama mbele zangu Musa na Samweli, moyo wangu usingewaelekea watu hawa; watupe, watoke mbele za macho yangu, wakaende zao. Kisha itakuwa, hapo watakapokuambia, Tutoke, tuende wapi? Utawaambia, BWANA asema hivi, Walioandikiwa kufa, watakwenda kufa; au kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga; au kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa, au kutekwa nyara, watakuwa mateka. Nami nitaamrisha juu yao namna nne, asema BWANA; upanga uue, na mbwa wararue, na ndege wa angani, na wanyama wakali wa nchi, wale na kuangamiza. Nami nitawafanya kuwa kitu cha kutisha katika falme zote za duniani, kwa sababu ya Manase, mwana wa Hezekia mfalme wa Yuda, kwa sababu ya mambo aliyoyatenda katika Yerusalemu.
Yeremia 15:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Yeremia 15:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kisha BWANA akaniambia: “Hata kama Musa na Samweli wangesimama mbele zangu, moyo wangu usingewaelekea watu hawa. Waondoe mbele za macho yangu! Waache waende! Nao wakikuuliza, ‘Twende wapi?’ Waambie, ‘Hili ndilo asemalo BWANA: “ ‘Wale waliowekwa kwa ajili ya kufa, na wafe; waliowekewa kufa kwa upanga, kwa upanga; waliowekewa kufa kwa njaa, kwa njaa; na waliowekewa kupelekwa uhamishoni, wapelekwe uhamishoni.’ ” BWANA asema, “Nitatuma aina nne za waangamizi: upanga ili kuua, mbwa ili kukokota mbali, ndege wa angani na wanyama wa nchi ili wale na waangamize. Nitawafanya wawe machukizo kwa falme zote za dunia kwa sababu ya kile alichofanya Manase mwana wa Hezekia mfalme wa Yuda huko Yerusalemu.