Yeremia 12:7-9
Yeremia 12:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nimeiacha nyumba yangu; nimeitupa mali yangu mimi mwenyewe. Israeli, mpenzi wangu wa moyo, nimemtia mikononi mwa maadui zake. Wateule wangu wamenigeuka, wamekuwa kama simba porini, wameningurumia mimi; ndiyo maana nawachukia. Wateule wangu wamekuwa ndege mzuri wanaoshambuliwa na kozi pande zote. Nenda ukawakusanye wanyama wote wakali waje kushiriki katika karamu.
Yeremia 12:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nimeiacha nyumba yangu, nimeutupa urithi wangu; nimemtia mpenzi wangu katika mikono ya adui zake. Urithi wangu umekuwa kwangu kama simba msituni; ameinua sauti yake juu yangu; kwa sababu hiyo nimemchukia. Je! Urithi wangu umekuwa kwangu kama ndege mwenye madoadoa? Ndege wakali wamemzunguka pande zote? Nendeni, wakusanyeni pamoja wanyama wote wa mwituni, waleteni ili wale.
Yeremia 12:7-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nimeiacha nyumba yangu, nimeutupa urithi wangu; nimemtia mpenzi wangu katika mikono ya adui zake. Urithi wangu umekuwa kwangu kama simba msituni; ameinua sauti yake juu yangu; kwa sababu hiyo nimemchukia. Je! Urithi wangu umekuwa kwangu kama ndege mwenye madoadoa? Ndege wakali wanamtulia pande zote? Enendeni, wakusanyeni pamoja wanyama wote wa mwituni, waleteni ili wale.
Yeremia 12:7-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Nitaiacha nyumba yangu, nitupe urithi wangu; nitamtia yeye nimpendaye mikononi mwa adui zake. Urithi wangu umekuwa kwangu kama simba wa msituni. Nauchukia kwa kuwa unaningurumia. Je, urithi wangu haukuwa kama ndege wa mawindo wa madoadoa ambaye ndege wengine wawindao humzunguka na kumshambulia? Nenda ukawakusanye pamoja wanyama wote wa mwituni; walete ili wale.