Yeremia 1:9-10
Yeremia 1:9-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha Mwenyezi-Mungu akaunyosha mkono wake, akagusa kinywa changu, akaniambia, “Tazama nimeyatia maneno yangu kinywani mwako. Leo nimekupa mamlaka juu ya mataifa na falme, uwe na mamlaka ya kungoa na kubomoa, mamlaka ya kuharibu na kuangamiza, mamlaka ya kujenga na ya kupanda.”
Yeremia 1:9-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo BWANA akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; BWANA akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako; angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.
Yeremia 1:9-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo BWANA akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; BWANA akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako; angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.
Yeremia 1:9-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kisha BWANA akaunyoosha mkono wake na kugusa kinywa changu, akaniambia, “Sasa nimeyaweka maneno yangu kinywani mwako. Tazama, leo nimekuweka juu ya mataifa na falme ili kungʼoa na kubomoa, kuharibu na kuangamiza, kujenga na kupanda.”