Yeremia 1:4-8
Yeremia 1:4-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu aliniambia neno lake: “Kabla hujachukuliwa mimba, mimi nilikujua, kabla hujazaliwa, mimi nilikuweka wakfu; nilikuteua uwe nabii kwa mataifa.” Nami nikajibu, Aa! Bwana Mwenyezi-Mungu, mimi sijui kusema, kwa kuwa bado ningali kijana. Lakini Mwenyezi-Mungu akaniambia, “Usiseme kwamba wewe ni kijana bado. Utakwenda kwa watu wote nitakaokutuma kwao, na yote nitakayokuamuru utayasema. Wewe usiwaogope watu hao, kwa maana niko pamoja nawe kukulinda. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Yeremia 1:4-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Neno la BWANA lilinijia, kusema, Kabla sijakuumba katika tumbo nilikujua, na kabla hujatoka tumboni, nilikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto. Lakini BWANA akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru. Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema BWANA.
Yeremia 1:4-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Neno la BWANA lilinijia, kusema, Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto. Lakini BWANA akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru. Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema BWANA.
Yeremia 1:4-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Neno la BWANA lilinijia, kusema, “Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako, nilikujua; kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalum; nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.” Nami nikasema, “Aa, BWANA Mwenyezi, sijui kusema, kwani mimi ni mtoto mdogo tu.” Lakini BWANA akaniambia, “Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utaenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza. Usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe,” asema BWANA.