Waamuzi 5:7-12
Waamuzi 5:7-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Wakulima walikoma kuwako, walikoma kuwako katika Israeli, mpaka nilipotokea mimi Debora, mimi niliye kama mama wa Israeli. Walijichagulia miungu mipya, kukawa na vita katika nchi. Lakini hakukupatikana mwenye upanga au ngao kati ya watu 40,000 wa Israeli. Nawapa heshima makamanda wa Israeli waliojitoa kwa hiari yao kati ya watu. Mshukuruni Mwenyezi-Mungu! “Tangazeni, enyi wapandapunda weupe, enyi mnaokalia mazulia ya fahari, nyinyi mnaotembea njiani, tangazeni jambo hilo. Imbeni kupita wanamuziki kwenye visima vya maji, tangazeni ushindi wa Mwenyezi-Mungu, ushindi kwa wakulima wake katika Israeli. Ndipo watu wa Mwenyezi-Mungu waliposhuka malangoni. “Amka, amka, Debora! Amka! Amka uimbe wimbo! Amka, Baraki mwana wa Abinoamu, uwachukue mateka wako.
Waamuzi 5:7-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Watawala walikoma katika Israeli, walikoma, Hadi mimi Debora nilipoinuka, Nilipoinuka mimi, mama katika Israeli. Walichagua miungu mipya, Ndipo kulikuwa na vita malangoni; Je! Ilionekana ngao au mkuki Katika watu elfu arubaini wa Israeli? Moyo wangu unawaelekea makamanda wa Israeli, Waliojitoa nafsi zao kwa hiari yao miongoni mwa watu; Mhimidini BWANA. Itangazeni habari, ninyi mpandao punda weupe, Ninyi mketio juu ya mazulia ya thamani, Na ninyi mnaopita njiani kwa miguu. Mbali na kelele za hao wapigao mishale, katika mahali pa kuteka maji, Hapo watatangaza matendo ya haki ya BWANA; Naam, matendo ya haki ya kutawala kwake katika Israeli. Ndipo watu wa BWANA waliposhuka malangoni. Amka, amka, Debora; Amka, amka, imba wimbo. Inuka, Baraka, wachukue mateka wao Waliokuchukua mateka, Ee mwana wa Abinoamu.
Waamuzi 5:7-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maliwali walikoma katika Israeli, walikoma, Hata mimi Debora nilipoinuka, Nilipoinuka mimi, mama katika Israeli. Walichagua miungu mipya, Ndipo kulikuwa na vita malangoni; Je! Ilionekana ngao au mkuki Katika watu elfu arobaini wa Israeli? Moyo wangu unawaelekea maliwali wa Israeli, Waliojitoa nafsi zao kwa hiari yao miongoni mwa watu; Mhimidini BWANA. Itangazeni habari, ninyi mpandao punda weupe, Ninyi mketio juu ya mazulia ya thamani, Na ninyi mnaopita njiani kwa miguu. Mbali na kelele za hao wapigao mishale, katika mahali pa kuteka maji, Hapo watatangaza matendo ya haki ya BWANA; Naam, matendo ya haki ya kutawala kwake katika Israeli. Ndipo watu wa BWANA waliposhuka malangoni. Amka, amka, Debora; Amka, amka, imba wimbo. Inuka, Baraka, wachukue mateka wao Waliokuchukua mateka, Ee mwana wa Abinoamu.
Waamuzi 5:7-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mashujaa walikoma katika Israeli, walikoma hadi mimi, Debora, nilipoinuka, nilipoinuka kama mama katika Israeli. Mungu alichagua viongozi wapya vita vilipokuja malangoni ya mji; lakini hapakuonekana ngao wala mkuki miongoni mwa watu elfu arobaini katika Israeli. Moyo wangu u pamoja na wakuu wa Israeli, u pamoja na wale wanaojitoa kwa hiari yao miongoni mwa watu. Mhimidini BWANA! “Ninyi mpandao punda weupe, mkiketi juu ya matandiko ya thamani, nanyi mnaotembea barabarani, fikirini kuhusu sauti za waimbaji mahali pa kunyweshea maji. Wanasimulia matendo ya haki ya BWANA, matendo ya haki ya mashujaa wake katika Israeli. “Ndipo watu wa BWANA walipoteremka malangoni pa mji. ‘Amka, amka! Debora! Amka, amka, uimbe! Ee Baraka! Inuka, chukua mateka wako uliowateka, ee mwana wa Abinoamu.’