Waamuzi 5:6-7
Waamuzi 5:6-7 Biblia Habari Njema (BHN)
“Katika siku za Shamgari, mwana wa Anathi, katika wakati wa Yaeli, misafara ilikoma kupita nchini, wasafiri walipitia vichochoroni. Wakulima walikoma kuwako, walikoma kuwako katika Israeli, mpaka nilipotokea mimi Debora, mimi niliye kama mama wa Israeli.
Waamuzi 5:6-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Katika siku za Shamgari, mwana wa Anathi, Siku za Yaeli, njia kuu zilikuwa hazina watu; Nayo misafara ilipita kwa njia za kando. Watawala walikoma katika Israeli, walikoma, Hadi mimi Debora nilipoinuka, Nilipoinuka mimi, mama katika Israeli.
Waamuzi 5:6-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Katika siku za Shamgari, mwana wa Anathi, Siku za Yaeli, njia kuu zilikuwa hazina watu; Nao wenye kusafiri walipita kwa njia za kando. Maliwali walikoma katika Israeli, walikoma, Hata mimi Debora nilipoinuka, Nilipoinuka mimi, mama katika Israeli.
Waamuzi 5:6-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Katika siku za Shamgari mwana wa Anathi, katika siku za Yaeli, barabara kuu hazikuwa na watu; wasafiri walipita njia za kando. Mashujaa walikoma katika Israeli, walikoma hadi mimi, Debora, nilipoinuka, nilipoinuka kama mama katika Israeli.