Waamuzi 4:9-10
Waamuzi 4:9-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Debora akamjibu, “Sawa. Nitakwenda pamoja nawe; lakini hutapata heshima yoyote ya ushindi, maana Mwenyezi-Mungu, atamtia Sisera mikononi mwa mwanamke.” Basi, Debora akafuatana na Baraki kwenda Kedeshi. Baraki akayaita makabila ya Naftali na Zebuluni huko Kedeshi; watu 10,000 wakamfuata. Debora akaenda pamoja naye.
Waamuzi 4:9-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi akasema, Hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini safari utakayoiendea haitakupatia heshima wewe; maana BWANA atamwuza Sisera katika mkono wa mwanamke. Debora akainuka, akaenda pamoja na Baraka mpaka Kedeshi. Baraka akawakutanisha Naftali na Zabuloni waende Kedeshi wakakwea watu elfu kumi wakimfuata; Debora naye akaenda pamoja naye.
Waamuzi 4:9-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi akasema, Hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini safari utakayoiendea haitakupatia heshima wewe; maana BWANA atamwuza Sisera katika mkono wa mwanamke. Debora akainuka, akaenda pamoja na Baraka mpaka Kedeshi. Baraka akawakutanisha Naftali na Zabuloni waende Kedeshi wakakwea watu elfu kumi wakimfuata; Debora naye akaenda pamoja naye.
Waamuzi 4:9-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Debora akamwambia, “Hakika nitaenda pamoja nawe, lakini njia unayoiendea haitakupa heshima wewe, kwa kuwa BWANA atamtia Sisera mikononi mwa mwanamke.” Hivyo Debora akaenda pamoja na Baraka hadi Kedeshi, ambapo Baraka aliwaita Zabuloni na Naftali. Watu elfu kumi wakamfuata Baraka, na Debora pia akaenda naye.