Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waamuzi 2:3-5 - Compare All Versions

Waamuzi 2:3-5 BHN (Biblia Habari Njema)

Kwa hiyo sasa nasema: Sitawafukuza tena wakazi wa nchi hii bali watawataabisha, nayo miungu yao itakuwa mtego kwenu.” Malaika wa Mwenyezi-Mungu alipowaambia watu wote wa Israeli maneno haya, walipaza sauti zao na kulia. Wakapaita mahali hapo Bokimu. Hapo wakamtolea sadaka Mwenyezi-Mungu.

Shirikisha
Waamuzi 2 BHN

Waamuzi 2:3-5 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni tanzi kwenu. Ikawa, hapo huyo malaika wa BWANA alipoyanena maneno haya, kuwaambia wana wa Israeli wote, ndipo hao watu wakainua sauti zao na kulia. Nao wakaliita jina la mahali pale Bokimu; nao wakamchinjia BWANA sadaka huko.

Shirikisha
Waamuzi 2 SUV

Waamuzi 2:3-5 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni mtego kwenu. Ikawa, hapo huyo malaika wa BWANA alipoyanena maneno haya, kuwaambia wana wa Israeli wote, ndipo hao watu wakainua sauti zao na kulia. Nao wakaliita jina la mahali pale Bokimu; nao wakamchinjia BWANA sadaka huko.

Shirikisha
Waamuzi 2 SRUV

Waamuzi 2:3-5 NEN (Neno)

Sasa basi ninawaambia kuwa sitawafukuza watoke kati yenu, ila watakuwa mitego kwenu, nayo miungu yao itakuwa tanzi kwenu.” Malaika wa BWANA alipomaliza kusema mambo haya kwa Waisraeli wote, watu wakalia kwa sauti kuu. Wakapaita mahali pale Bokimu. Nao wakamtolea BWANA sadaka.

Shirikisha
Waamuzi 2 NEN