Waamuzi 2:15-16
Waamuzi 2:15-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Kila walipokwenda kupigana, mkono wa Mwenyezi-Mungu uliwakabili kuwaletea balaa, kama alivyokuwa amewaonya na kuapa. Nao wakawa katika huzuni kubwa. Ndipo Mwenyezi-Mungu akawapa waamuzi ambao waliwaokoa mikononi mwa watu waliopora mali zao.
Waamuzi 2:15-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kila walikokwenda mkono wa BWANA ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama BWANA alivyosema, na kama BWANA alivyowaapia; nao wakafadhaika sana. Kisha BWANA akawainua waamuzi, waliowaokoa mikononi mwa watu hao waliowateka nyara.
Waamuzi 2:15-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kila walikokwenda mkono wa BWANA ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama BWANA alivyosema, na kama BWANA alivyowaapia; nao wakafadhaika sana. Kisha BWANA akawainua waamuzi, waliowaokoa na mikono ya watu hao waliowateka nyara.
Waamuzi 2:15-16 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wakati wowote Israeli walipotoka kwenda kupigana, mkono wa BWANA ulikuwa kinyume nao ili awashinde, kama vile alivyokuwa amewaapia. Nao wakawa katika taabu kubwa. Ndipo BWANA akawainua waamuzi, ambao waliwaokoa kutoka mikononi mwa hao wavamizi.