Waamuzi 15:14-15
Waamuzi 15:14-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Alipofika Lehi, Wafilisti walimwendea mbio huku wakipiga kelele. Ghafla roho ya Mwenyezi-Mungu ikamjia Samsoni kwa nguvu na zile kamba walizomfunga mikononi mwake zikakatika kama kitani kilichoshika moto, navyo vifungo vikaanguka chini. Samsoni akapata utaya mbichi wa punda, akautumia kuwaua watu 1,000.
Waamuzi 15:14-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Alipofika Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo Roho ya BWANA ikamjia kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake. Naye akaona mfupa mbichi wa taya ya punda, akautwaa, akaua watu elfu moja kwa mfupa huo
Waamuzi 15:14-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Alipofika Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo roho ya BWANA ikamjia kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake. Naye akaona mfupa mbichi wa taya ya punda, akautwaa, akapiga watu elfu kwa mfupa huo
Waamuzi 15:14-15 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Alipokaribia Lehi, Wafilisti wakamjia wakipiga kelele. Roho wa BWANA akaja juu yake kwa nguvu. Kamba zilizomfunga mikono zikawa kama kitani iliyochomwa kwa moto, na vifungo vyake vikaanguka chini toka mikononi mwake. Ndipo akaona mfupa mpya wa taya la punda, akanyoosha mkono, akauchukua na kuua nao Wafilisti wapatao elfu moja.