Waamuzi 13:18-20
Waamuzi 13:18-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Malaika wa Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Kwa nini unataka kujua jina langu, kwa kuwa jina langu ni la ajabu?” Hapo Manoa akatayarisha mwanambuzi na tambiko, akaviweka juu ya mwamba amtolee Mwenyezi-Mungu afanyaye maajabu. Basi, wakati Manoa na mkewe walipokuwa wanatazama miali ya moto ikipanda juu mbinguni kutoka madhabahuni, walimwona malaika katika miali hiyo akipanda kwenda mbinguni. Basi Manoa na mkewe wakasujudu.
Waamuzi 13:18-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Huyo malaika wa BWANA akamwambia, Kwa nini unaniuliza jina langu, na jina hilo ni la ajabu? Basi Manoa akamtwaa yule mwana-mbuzi, pamoja na sadaka ya unga, akamtolea BWANA hapo juu ya mwamba; huyo malaika akatenda la ajabu; Manoa na mkewe wakaangalia. Kwa maana, ikawa, mara huo muali wa moto ulipopaa juu mbinguni kutoka pale madhabahuni, huyo malaika wa BWANA akapaa katika mwali wa moto wa madhabahu; nao Manoa na mkewe wakaangalia; wakaanguka kifudifudi.
Waamuzi 13:18-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Huyo malaika wa BWANA akamwambia, Kwani wewe kuniuliza jina langu, kwa kuwa jina hilo ni la ajabu? Basi Manoa akamtwaa yule mwana-mbuzi, pamoja na sadaka ya unga, akamtolea BWANA hapo juu ya mwamba; huyo malaika akatenda la ajabu; Manoa na mkewe wakaangalia. Kwa maana, ikawa, mara huo mwali wa moto ulipopaa juu mbinguni kutoka pale madhabahuni, huyo malaika wa BWANA akapaa katika mwali wa moto wa madhabahu; nao Manoa na mkewe wakaangalia; wakainama kifudifudi.
Waamuzi 13:18-20 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Malaika wa BWANA akamjibu, “Kwa nini unauliza jina langu? Ni jina la ajabu.” Ndipo Manoa akamchukua mwana-mbuzi, pamoja na sadaka ya unga, naye akamtolea BWANA dhabihu hapo juu ya mwamba. Naye yule malaika wa BWANA akafanya jambo la ajabu wakati Manoa na mkewe wakiwa wanaangalia: Mwali wa moto kutoka hapo madhabahuni ulipowaka kuelekea mbinguni, malaika wa BWANA akapaa ndani ya huo mwali. Manoa na mkewe, kwa kuona jambo hili, wakaanguka kifudifudi.