Waamuzi 1:29-30
Waamuzi 1:29-30 Biblia Habari Njema (BHN)
Watu wa kabila la Efraimu hawakuwafukuza Wakanaani walioishi huko Gezeri, na hawa waliishi huko pamoja na watu wa Efraimu. Watu wa kabila la Zebuluni hawakuwafukuza wakazi wa mji wa Kitroni, wala wale wa mji wa Nahalali, waliendelea kukaa pamoja nao wakiwafanyiza kazi za kulazimishwa.
Waamuzi 1:29-30 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Efraimu naye hakuwatoa Wakanaani waliokuwa wakikaa katika Gezeri; lakini Wakanaani walikaa ndani ya Gezeri kati yao. Zabuloni naye hakuwatoa wenyeji wa Kitroni, wala hao waliokaa katika Nahalali; lakini Wakanaani walikaa kati yao, wakalazimishwa shokoa.
Waamuzi 1:29-30 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Efraimu naye hakuwatoa Wakanaani waliokuwa wakikaa katika Gezeri; lakini Wakanaani walikaa ndani ya Gezeri kati yao. Zabuloni naye hakuwatoa wenyeji wa Kitroni, wala hao waliokaa katika Nahalali; lakini Wakanaani walikaa kati yao, wakalazimishwa shokoa.
Waamuzi 1:29-30 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wala Efraimu hawakuwafukuza kabisa Wakanaani walioishi Gezeri, bali Wakanaani waliendelea kuishi miongoni mwao. Vivyo hivyo Zabuloni hawakuwafukuza Wakanaani walioishi huko Kitroni, na walioishi Nahaloli, bali Wakanaani hao walibaki miongoni mwao; lakini waliwatia katika kazi ya kulazimishwa.