Yakobo 5:7-9
Yakobo 5:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Basi, ndugu zangu, muwe na subira mpaka Bwana atakapokuja. Tazameni mkulima anavyongoja kwa subira mimea yake itoe mavuno ya thamani. Yeye hungojea kwa subira mvua za masika na za vuli. Nanyi pia mnapaswa kuwa na subira; imarisheni mioyo yenu, maana siku ya kuja kwake Bwana inakaribia. Ndugu zangu, msinung'unikiane nyinyi kwa nyinyi msije mkahukumiwa na Mungu. Hakimu yu karibu, tayari kuingia.
Yakobo 5:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia. Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.
Yakobo 5:7-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia. Ndugu, msinung’unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.
Yakobo 5:7-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa hiyo, ndugu zangu, vumilieni hadi kuja kwake Bwana. Tazameni jinsi mkulima angojavyo ardhi itoe mavuno yake yaliyo ya thamani, na jinsi anavyovumilia kwa ajili ya kupata mvua ya kwanza na ya mwisho. Ninyi nanyi vumilieni, tena simameni imara, kwa sababu kuja kwa Bwana kumekaribia. Ndugu zangu, msinungʼunikiane, msije mkahukumiwa. Hakimu amesimama mlangoni!