Yakobo 3:17-18
Yakobo 3:17-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini hekima itokayo juu mbinguni, kwanza ni safi; inapenda amani, upole na huwajali watu; imejaa huruma na huzaa matunda ya matendo mema; haina ubaguzi wala unafiki. Uadilifu ni mazao ya mbegu ambazo wapenda amani hupanda katika amani.
Yakobo 3:17-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.
Yakobo 3:17-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.
Yakobo 3:17-18 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Lakini hekima inayotoka mbinguni kwanza ni safi, kisha inapenda amani, tena ni ya upole, iliyo tayari kusikiliza wengine kwa unyenyekevu, iliyojaa huruma na matunda mema, isiyopendelea mtu, tena isiyokuwa na unafiki. Mavuno ya haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.