Yakobo 2:8-12
Yakobo 2:8-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Kama mnaitimiza ile sheria ya ufalme kama ilivyoandikwa katika Maandiko Matakatifu: “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe”, mtakuwa mnafanya vema kabisa. Lakini mkiwabagua watu, basi, mwatenda dhambi, nayo sheria inawahukumu nyinyi kuwa mna hatia. Anayevunja amri mojawapo ya sheria, atakuwa na hatia ya kuivunja sheria yote. Maana yuleyule aliyesema: “Usizini,” alisema pia “Usiue.” Kwa hiyo, hata ikiwa hukuzini, lakini umeua, wewe umeivunja sheria. Basi, semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria iletayo uhuru.
Yakobo 2:8-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema. Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria kuwa wakosaji. Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria. Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru.
Yakobo 2:8-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema. Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria kuwa wakosaji. Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria. Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru.
Yakobo 2:8-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kama kweli mnaitimiza ile sheria ya kifalme inayopatikana katika Maandiko, isemayo, “Mpende jirani yako kama unavyoipenda nafsi yako,” mnafanya vyema. Lakini mkiwapendelea watu, mnatenda dhambi, na sheria inawahukumu kuwa wakosaji. Kwa maana mtu yeyote anayeishika sheria yote lakini akajikwaa katika kipengele kimoja tu, ana hatia ya kuivunja sheria yote. Kwa sababu yeye aliyesema, “Usizini,” alisema pia, “Usiue.” Basi kama huzini lakini unaua, umekuwa mvunjaji wa sheria. Hivyo semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ile iletayo uhuru.