Yakobo 2:24-26
Yakobo 2:24-26 Biblia Habari Njema (BHN)
Mnaona, basi, kwamba mtu hukubaliwa kuwa mwadilifu kwa matendo yake, na si kwa imani peke yake. Ilikuwa vivyo hivyo kuhusu yule malaya Rahabu; yeye alikubaliwa kuwa mwadilifu kwa sababu aliwapokea wale wapelelezi na kuwasaidia waende zao kwa kupitia njia nyingine. Basi, kama vile mwili bila roho umekufa, vivyo hivyo imani bila matendo imekufa.
Yakobo 2:24-26 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake. Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine? Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.
Yakobo 2:24-26 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake. Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine? Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.
Yakobo 2:24-26 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mnaona kwamba mtu huhesabiwa haki kwa yale anayotenda wala si kwa imani peke yake. Vivyo hivyo, hata Rahabu, yule kahaba: je, hakuhesabiwa haki kwa yale aliyotenda alipowapokea wale wapelelezi na kuwaambia waende njia nyingine? Kama vile mwili pasipo roho umekufa, kadhalika nayo imani pasipo matendo imekufa.