Isaya 9:8-10
Isaya 9:8-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu ametoa tamko dhidi ya Yakobo nalo litampata Israeli. Watu wote watatambua, ukoo wote wa Efraimu na wakazi wa Samaria. Kwa kiburi na majivuno wanasema: “Kuta za matofali zimeanguka lakini sisi tutazijenga kwa mawe yaliyochongwa! Nyumba za boriti za mikuyu zimeharibiwa lakini mahali pake tutajenga za mierezi.”
Isaya 9:8-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Bwana alimpelekea Yakobo neno, nalo likamfikia Israeli. Nao watu wote watajua, yaani, Efraimu na yeye akaaye Samaria, wasemao kwa kiburi na kwa kujisifu nafsi zao, Matofali yameanguka, lakini sisi tutajenga kwa mawe yaliyochongwa; mikuyu imekatwa lakini sisi tutaweka mierezi badala yake.
Isaya 9:8-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Bwana alimpelekea Yakobo neno, likamfikilia Israeli. Nao watu wote watajua, yaani, Efraimu na yeye akaaye Samaria, wasemao kwa kiburi na kwa kujisifu nafsi zao, Matofali yameanguka, lakini sisi tutajenga kwa mawe yaliyochongwa; mikuyu imekatwa lakini sisi tutaweka mierezi badala yake.
Isaya 9:8-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Bwana ametuma ujumbe dhidi ya Yakobo, utamwangukia Israeli. Watu wote watajua hili: Efraimu na wakazi wa Samaria, wanaosema kwa kiburi na majivuno ya mioyo, “Matofali yameanguka chini, lakini tutajenga tena kwa mawe yaliyochongwa, mikuyu imekatwa, na tutapanda mierezi badala yake.”