Isaya 8:14-18
Isaya 8:14-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Mimi nitakuwa kimbilio, nitakuwa pia kama jiwe la kujikwaa, mwamba wa kuziangusha falme za Israeli na Yuda; nitakuwa mtego wa kuwatega na kuwanasa wakazi wa Yerusalemu. Watu wengi watajikwaa, wataanguka na kupondeka; watanaswa katika mtego huo na kuchukuliwa mateka.” Nitalihifadhi agizo hilo na kulifunga fundisho hilo miongoni mwa wafuasi wangu. Nitamngojea Mwenyezi-Mungu ambaye amejificha mbali na wazawa wa Yakobo; nitamtumainia. Mimi pamoja na watoto alionipa Mwenyezi-Mungu ni ishara na alama katika Israeli kwa jina la Mwenyezi-Mungu wa majeshi akaaye mlimani Siyoni.
Isaya 8:14-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu. Na wengi watajikwaa juu yake, na kuanguka na kuvunjika, na kunaswa na kukamatwa. Ufunge huo ushuhuda, ukaitie mhuri sheria kati ya wanafunzi wangu. Nami nitamngojea BWANA, awafichaye uso wake nyumba ya Yakobo, nami nitamtazamia. Angalieni, mimi na watoto hawa niliopewa na BWANA tu ishara na ajabu katika Israeli, zitokazo kwa BWANA wa majeshi, yeye akaaye katika mlima Sayuni.
Isaya 8:14-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu. Na wengi watajikwaa juu yake, na kuanguka na kuvunjika, na kunaswa na kukamatwa. Ufunge huo ushuhuda, ukaitie muhuri sheria kati ya wanafunzi wangu. Nami nitamngojea BWANA, awafichaye uso wake nyumba ya Yakobo, nami nitamtazamia. Angalieni, mimi na watoto hawa niliopewa na BWANA tu ishara na ajabu katika Israeli, zitokazo kwa BWANA wa majeshi, yeye akaaye katika mlima Sayuni.
Isaya 8:14-18 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
naye atakuwa mahali patakatifu; lakini kwa nyumba zote mbili za Israeli atakuwa jiwe lile linalosababisha watu kujikwaa na mwamba wa kuwaangusha. Kwa watu wa Yerusalemu, atakuwa mtego na tanzi. Wengi wao watajikwaa; wataanguka na kuvunjika, watategwa na kunaswa.” Funga ushuhuda na kutia muhuri sheria miongoni mwa wanafunzi wangu. Nitamngojea BWANA, ambaye ameificha nyumba ya Yakobo uso wake. Nitaliweka tumaini langu kwake. Niko hapa, pamoja na watoto ambao BWANA amenipa. Sisi ni ishara na mfano wake katika Israeli, kutoka kwa BWANA wa majeshi, anayeishi juu ya Mlima Sayuni.