Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 65:1-16

Isaya 65:1-16 Biblia Habari Njema (BHN)

Mwenyezi-Mungu asema; “Nilikuwa tayari kujionesha kwao wasiouliza habari zangu. Nilikuwa tayari kuwapokea wale wasionitafuta. Nililiambia taifa ambalo halikuomba kwa jina langu: ‘Nipo hapa! Nipo hapa!’ Mchana kutwa niliwanyoshea mikono watu waasi, watu ambao hufuata njia zisizo sawa, watu ambao hufuata fikira zao wenyewe. Ni watu ambao daima hunichokoza waziwazi; hutambikia miungu yao katika bustani, na kuifukizia ubani juu ya matofali. Huketi makaburini na kukaa mafichoni usiku. Hula nyama ya nguruwe na mchuzi wa wanyama haramu. Huwaambia wale wanaokutana nao: ‘Kaeni mbali nami; msinikaribie kwani mimi ni mtakatifu!’ Watu hao wananikasirisha mno, hasira yangu ni kama moto usiozimika. “Jueni kuwa nimelitia jambo hilo moyoni, sitanyamaza bali nitawafanya walipe; nitawafanya walipe kwa wingi. Mimi Mwenyezi-Mungu, nitawalipiza maovu yao wayalipie na maovu ya wazee wao. Wao waliifukizia ubani miungu yao milimani, wakanitukana mimi huko vilimani. Nitawafanya walipe kwa wingi, watayalipia matendo yao ya awali.” Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mtu akikuta kishada cha zabibu nzuri, watu husema: ‘Tusikiharibu; kina baraka.’ Ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu; sitawaangamiza wote. Nitawajalia watu wa Yakobo, na Yuda nitamjalia warithi wa milima yangu; watumishi wangu watakaa huko. Nchi tambarare ya Sharoni itakuwa malisho, bonde la Akori litakuwa mapumziko ya mifugo kwa ajili ya watu wangu walionitafuta. “Lakini nitafanya nini na nyinyi mnaoniacha mimi Mwenyezi-Mungu, msioujali Siyoni, mlima wangu mtakatifu, nyinyi mnaoabudu mungu ‘Gadi’, na kumtolea tambiko ya divai mungu ‘Meni’? Nimewapangia kifo kwa upanga, nyote mtaangukia machinjoni! Maana, nilipowaita, hamkuniitikia; niliponena, hamkunisikiliza. Mlitenda yaliyo maovu mbele yangu, mkachagua yale nisiyoyapenda. Basi, mimi Mwenyezi-Mungu nasema, watumishi wangu watakula, lakini nyinyi mtaona njaa; watumishi wangu watakunywa, lakini nyinyi mtaona kiu; watumishi wangu watafurahi, lakini nyinyi mtafedheheka. Watumishi wangu wataimba kwa furaha moyoni, lakini nyinyi mtalia kwa uchungu moyoni na kupiga kelele kwa uchungu mkubwa rohoni. Wale niliowachagua nitawapa jina jipya. Lakini nyinyi jina lenu watalitumia kulaania; ‘Watasema: Bwana Mungu awaue kama hao.’ Basi, mwenye kujitakia baraka nchini, atajitakia baraka kwa Mungu wa kweli. Mwenye kuapa katika nchi hii, ataapa kwa Mungu wa kweli. Maana taabu za zamani zimepita zimetoweka kabisa mbele yangu.

Shirikisha
Soma Isaya 65

Isaya 65:1-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Watu wasionitaka wanauliza habari zangu; nimeonekana na hao wasionitafuta; nililiambia taifa lisiloitwa kwa jina langu, Nitazameni, nitazameni. Mchana kutwa nimewanyoshea mikono yangu watu walioasi, watu waendao katika njia isiyo njema, wakifuata mawazo yao wenyewe; watu wanikasirishao mbele za uso wangu daima, wakitoa dhabihu katika bustani zao, na kufukiza uvumba juu ya matofali; waketio kati ya makaburi, na kulala katika mahali pao pa siri; walao nyama ya nguruwe, na mchuzi wa vitu vinichukizavyo u katika vyombo vyao; watu wasemao, Simama peke yako, usinikaribie mimi, kwa maana mimi ni mtakatifu kuliko wewe; watu hao ni moshi puani mwangu, moto uwakao mchana kutwa. Tazama, neno hili limeandikwa mbele zangu. Sitanyamaza, lakini nitalipa, naam, mimi nitawalipa ujira wao vifuani mwao; maovu yenu na maovu ya baba zenu pamoja, asema BWANA, ninyi mliofukiza uvumba juu ya milima, na kunitukana juu ya vilima; basi, kwa ajili ya hayo nitawapimia kwanza kazi yao vifuani mwao. BWANA asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, Usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake; ndivyo nitakavyotenda kwa ajili ya watumishi wangu, ili nisiwaharibu wote. Nami nitaleta uzao toka Yakobo, na mrithi wa milima yangu toka Yuda, na mteule wangu atairithi, na watumishi wangu watakaa huko. Na Sharoni itakuwa zizi la makundi ya kondoo, na bonde la Akori mahali pa kulala makundi ya ng'ombe, kwa ajili ya watu wangu walionitafuta. Bali ninyi mmwachao BWANA, na kuusahau mlima wangu mtakatifu, na kuandaa meza kwa ajili ya Bahati, na kuijazia Ajali vyombo vya divai iliyochanganyika; mimi nitawaandikia kuuawa kwa upanga, na ninyi nyote mtainama ili kuchinjwa; kwa sababu nilipoita hamkuitika; niliponena, hamkusikia; bali mlitenda yaliyo mabaya machoni pangu, mlichagua mambo nisiyoyafurahia. Kwa hiyo Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, watumishi wangu watakula, bali ninyi mtaona njaa; tazama, watumishi wangu watakunywa, bali ninyi mtaona kiu; tazama, watumishi wangu watafurahi, bali ninyi mtatahayarika; tazama, watumishi wangu wataimba kwa furaha ya moyo, bali ninyi mtalia kwa huzuni ya moyo; mtapiga kelele kwa sababu ya uchungu wa roho zenu. Nanyi mtaliacha jina lenu kuwa laana kwa wateule wangu. Na Bwana MUNGU atakuua; naye atawaita watumishi wake kwa jina lingine. Hata itakuwa yeye atakayejibariki duniani, atajibariki kwa Mungu wa kweli; naye atakayeapa duniani, ataapa kwa Mungu wa kweli. Kwa kuwa taabu za kwanza zimesahauliwa, na kwa kuwa zimefichwa machoni pangu.

Shirikisha
Soma Isaya 65

Isaya 65:1-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Watu wasionitaka wanauliza habari zangu; nimeonekana na hao wasionitafuta; naliliambia taifa lisiloitwa kwa jina langu, Nitazameni, nitazameni. Mchana kutwa nimewanyoshea mikono yangu watu walioasi, watu waendao katika njia isiyo njema, wakifuata mawazo yao wenyewe; watu wanikasirishao mbele za uso wangu daima, wakitoa dhabihu katika bustani zao, na kufukiza uvumba juu ya matofali; waketio kati ya makaburi, na kulala katika mahali pao pa siri; walao nyama ya nguruwe, na mchuzi wa vitu vinichukizavyo u katika vyombo vyao; watu wasemao, Simama peke yako, usinikaribie mimi, kwa maana mimi ni mtakatifu kuliko wewe; watu hao ni moshi puani mwangu, moto uwakao mchana kutwa. Tazama, neno hili limeandikwa mbele zangu. Sitanyamaza, lakini nitalipa, naam, mimi nitawalipa ujira wao vifuani mwao; maovu yenu na maovu ya baba zenu pamoja, asema BWANA, ninyi mliofukiza uvumba juu ya milima, na kunitukana juu ya vilima; basi, kwa ajili ya hayo nitawapimia kwanza kazi yao vifuani mwao. BWANA asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, Usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake; ndivyo nitakavyotenda kwa ajili ya watumishi wangu, ili nisiwaharibu wote. Nami nitaleta uzao toka Yakobo, na mrithi wa milima yangu toka Yuda, na mteule wangu atairithi, na watumishi wangu watakaa huko. Na Sharoni itakuwa zizi la makundi ya kondoo, na bonde la Akori mahali pa kulala makundi ya ng’ombe, kwa ajili ya watu wangu walionitafuta. Bali ninyi mmwachao BWANA, na kuusahau mlima wangu mtakatifu, na kuandika meza kwa ajili ya Bahati, na kuijazia Ajali vyombo vya divai iliyochanganyika; mimi nitawaandikia kuuawa kwa upanga, na ninyi nyote mtainama ili kuchinjwa; kwa sababu nilipoita hamkuitika; niliponena, hamkusikia; bali mlitenda yaliyo mabaya machoni pangu, mlichagua mambo nisiyoyafurahia. Kwa hiyo Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, watumishi wangu watakula, bali ninyi mtaona njaa; tazama, watumishi wangu watakunywa, bali ninyi mtaona kiu; tazama, watumishi wangu watafurahi, bali ninyi mtatahayarika; tazama, watumishi wangu wataimba kwa furaha ya moyo, bali ninyi mtalia kwa huzuni ya moyo; mtapiga kelele kwa sababu ya uchungu wa roho zenu. Nanyi mtaliacha jina lenu kuwa laana kwa wateule wangu. Na Bwana MUNGU atakuua; naye atawaita watumishi wake kwa jina lingine. Hata itakuwa yeye atakayejibariki duniani, atajibariki kwa Mungu wa kweli; naye atakayeapa duniani, ataapa kwa Mungu wa kweli. Kwa kuwa taabu za kwanza zimesahauliwa, na kwa kuwa zimefichwa machoni pangu.

Shirikisha
Soma Isaya 65

Isaya 65:1-16 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

“Nilijifunua kwa watu wale ambao hawakuniulizia. Nimeonekana na watu wale ambao hawakunitafuta. Kwa taifa lile ambalo halikuliita Jina langu, nilisema, ‘Niko hapa, niko hapa.’ Mchana kutwa nimeinyoosha mikono yangu kwa watu wakaidi, wanaokwenda katika njia ambazo si nzuri, wafuatao mawazo yao wenyewe: taifa ambalo daima hunikasirisha machoni pangu, wakitoa dhabihu katika bustani na kufukiza uvumba juu ya madhabahu za matofali; watu waketio katikati ya makaburi na kukesha mahali pa siri, walao nyama za nguruwe, nazo sufuria zao zina mchuzi wa nyama zilizo najisi, wasemao, ‘Kaa mbali; usinikaribie, kwa maana mimi ni mtakatifu mno kwako!’ Watu wa aina hiyo ni moshi katika pua zangu, ni moto uwakao mchana kutwa. “Tazama, jambo hili hubakia limeandikwa mbele zangu: sitanyamaza, bali nitalipiza kwa ukamilifu; nitalipiza mapajani mwao: dhambi zenu na dhambi za baba zenu,” asema BWANA. “Kwa sababu walitoa dhabihu za kuteketezwa juu ya milima na kunichokoza mimi juu ya vilima, nitawapimia mapajani mwao malipo makamilifu kwa matendo yao ya zamani.” Hili ndilo asemalo BWANA: “Kama vile divai mpya ingali bado inapatikana katika kishada cha zabibu, nao watu husema, ‘Usikiharibu, kwa kuwa bado kuna kitu kizuri ndani yake,’ hivyo ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu; sitawaangamiza wote. Nitawaleta wazao kutoka kwa Yakobo, na kutoka kwa Yuda wale watakaomiliki milima yangu, nao watu wangu wateule watairithi, nako huko wataishi watumishi wangu. Sharoni itakuwa malisho kwa ajili ya makundi ya kondoo, na Bonde la Akori mahali pa kupumzikia kwa makundi ya ngʼombe, kwa ajili ya watu wangu wanaonitafuta. “Bali kwenu ninyi mnaomwacha BWANA na kuusahau mlima wangu mtakatifu, ninyi mnaoandaa meza kwa ajili ya Bahati, na kujaza mabakuli ya mvinyo uliochanganywa kwa ajili ya Ajali, nitawaagiza mfe kwa upanga, nanyi nyote mtainama chini ili kuchinjwa; kwa kuwa niliwaita lakini hamkuitika, nilisema lakini hamkusikiliza. Mlitenda maovu machoni pangu, nanyi mkachagua mambo yale yanayonichukiza.” Kwa hiyo hili ndilo asemalo BWANA Mwenyezi: “Watumishi wangu watakula, lakini ninyi mtaona njaa; watumishi wangu watakunywa lakini ninyi mtaona kiu; watumishi wangu watafurahi, lakini ninyi mtaona haya. Watumishi wangu wataimba kwa furaha ya mioyo yao, lakini ninyi mtalia kutokana na uchungu wa moyoni, na kupiga yowe kwa sababu ya uchungu wa roho zenu. Mtaliacha jina lenu kuwa laana kwa watu wangu waliochaguliwa; BWANA Mwenyezi atawaua ninyi, lakini watumishi wake atawapa jina jingine. Yeye aombaye baraka katika nchi atafanya hivyo kwa Mungu wa kweli; yeye aapaye katika nchi ataapa kwa Mungu wa kweli. Kwa kuwa taabu za zamani zitasahaulika na kufichwa kutoka machoni pangu.

Shirikisha
Soma Isaya 65

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha