Isaya 64:8-9
Isaya 64:8-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Hata hivyo, ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni Baba yetu. Sisi ni kama udongo, wewe ni mfinyanzi. Sisi sote ni kazi ya mikono yako. Usitukasirikie mno, ee Mwenyezi-Mungu, usiukumbuke uovu wetu daima! Ukumbuke kwamba sisi sote ni watu wako!
Isaya 64:8-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini sasa, Ee BWANA, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako. Ee BWANA, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu wako.
Isaya 64:8-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini sasa, Ee BWANA, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako. Ee BWANA, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu wako.
Isaya 64:8-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Lakini, Ee BWANA, wewe ndiwe Baba yetu. Sisi ni udongo, na wewe ndiwe mfinyanzi; sisi sote tu kazi ya mkono wako. Ee BWANA, usikasirike kupita kiasi, usizikumbuke dhambi zetu milele. Ee Bwana, utuangalie, twakuomba, kwa kuwa sisi sote tu watu wako.